top of page

CHACHU YA KALE!

Updated: Sep 2, 2022



“Chachu ya kale/Old yeast.”



“  Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.” 1 Wakorintho 5:7-8

“Chachu” ni jamaii ya mmea fulani (yellowish froth produced by fermenting malt worts) kawaida chachu utumika kutengenezea  ``hamira” /Au ndio hamira yenyewe . Chachu hutumika kwenye mikate,kwenye bia,na kwenye baadhi ya madawa. Kazi yake kubwa ni kuchachua kitu. Tazama mfano wa kazi ya hamira inayotumia kwenye  vyakula kama vile ugali, maandazi,mikate,chapati,n.k


Utagundua kwamba chakula kidogo kabla ya kutengenezwa kikichachushwa kinakuwa kikubwa,mfano pale unapotia hamira kwenye unga wa ngano. Neno hili “chachu” kwenye biblia limetumika kuashilia “uharibifu,uovu na ubaya,” Kwa mfano chachu ya Mafarisayo ilikuwa ni “unafiki” -Luka 12:1


Kipindi cha Waisraeli pale walipokuwa wamekaribia sana kutoka Misri,walipewa maelekezo muhimu yatakayo wawezesha kutoka salama. Moja kati ya maelekezo ya Kiungu hayo ni kutokutumia “chachu”  kabisa katika makao yao yote kwa muda wa siku saba,na endapo yeyote katika wana wa Israeli angelionekana ametumia chachu katika kipindi hicho basi adhabu yake itakuwa ni kukatiliwa mbali na kusanyiko la Israeli yaani angelitengwa mbali na ukombozi (Kutoka 12:19-20).


Bila shaka Mungu alikuwa akiwafundisha utii na nidhamu,lakini kwa nini chachu?. Chachu kama chachu ilifanya chakula kiharibike kwa wepesi,kisiwe na radha hasilia,lakini pia Chachu ilibeba ufunuo mkubwa katika agano jipya,ufunuo huo upo katika maeneo mawili;

,kwanza ni ``katika Neno la Bwana”,kwamba kama mwamini katika Kristo,hutakiwi kula Neno lililoghoshiwa/lililo na chachu/lililochakachuliwa,kwa maana hutaweza kukua kiroho (1 Petro 2:2),


Hivyo Neno likiwa na chachu,halifai kwa maana mbali na kuleta uharibifu kwenye afya ya kiroho ya mwamini lakini pia linamtenga mtu na uwepo wa Kristo,

Tunaposema neno lililo na chachu ni lile lililochakachuliwa kwa kutafsiriwa kinyume na lilivyo,kuongeza au kupunguza kile alichokusudia Bwana.Lakini pili ni katika eneo la unafiki/ubaya au uharibifu.Kwa maana yeyote katika kusanyiko la Bwana atakayekuwa ni mharibifu atatengwa mbali na kusanyiko.

Sasa,Paulo anasema kitu cha maana sana (kwenye andiko la 1 Wakorintho 5:7-8,lililopo hapo juu),kwamba  wale walio ndani ya Kristo,hawana budi kuweka mbali kila aina ya chachu kwa maana hata chachu ndogo ikiwa watakuwa nayo basi ni dhahiri kabisa chachu hiyo ndogo huchachua donge zima. (Uharibifu mdogo husababisha mengi kuharibika). Ebu fikiria,ikiwa kama mtu atashikilia uharibifu mdogo,


hali anatembea na Mungu,basi ukweli ni kwamba uharibifu huo utasababisha kuharibika kwa mengi aliyokuwa nayo.(Kumbuka;Chachu ya kale ni utu wa kale wenye uharibifu wa kila namna ambapo kama mtu akiingia nao kwenye wokovu,utamsumbua sana.)

Biblia inaposema“itoeni chachu ya kale,…” ina maana uwezo wa kuzitoa chachu hizo upo ndani yetu,ndio maana tunaambiwa tutoe.


Watu wengi bado wanashikilia chachu za kale. Hatua ya kuwa donge jipya ni hatua inayomwitaji Mungu lakini pia inakuhitaji wewe,hivyo Mungu ana sehemu yake na wewe una sehemu yako.

Paulo anasema wewe hukutiwa chachu ndani ya Kristo,yaani ndani ya Kristo hukupewa uharibifu wa aina yoyote maana ndivyo ilivyo,ndani Yake kuna ukamilifu. “Weupe wa moyo na kweli” ndio dhana ya maana inayokusudiwa kwako,na inawezekana kufikia hapo,ikiwa kama utakubali leo kuicha chachu ya kale!.


Namna ya kuacha chachu ya kale,ni kujisalimisha tena kwa Kristo kwa njia ya toba,tena kujenga shauku ya kuichukia chachu ya kale ambayo ni uharibifu wa kila namna,ukiombewa ujue ile nguvu ya chachu uondoka,na hatimaye kuanza safari ya kuelekea kwenye donge jipya na kweli.


Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI


kwa maana nawe unapitia changamoto hii,Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900


What’s app namba ni +255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

Commenti


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page