BWANA ATAKUPANDISHA KUTOKA JAANI.
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 7, 2015
- 2 min read
Updated: Sep 5, 2022

“ Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.” Zab.113:7
Andiko hili la Zaburi linaeleza hasa huruma ya Bwana juu ya watu wake na hasa wale wahitaji waliokosa msaada lakini mioyoni mwao wakimtegemea Bwana. Lakini wakati mwingine watu hao hao,wanajikuta wapo mbali na Bwana,lakini kwa huruma tu ya Bwana,anashughulika nao kana kwamba walimwomba. Ukweli ni kwamba kuinuliwa si jambo ambalo walistahili lakini neema ya Bwana inawasaidia hata Bwana kuwainua.Kiwango cha njaa unayoipitia,Yeye anaijua wala vizuri,kwa huruma zake,anakuinua.
Lakini kwa nini unapitia hali duni kama hiyo?
Majibu yanaweza yakawa mengi sana,lakini kwa mujibu wa Neno la Mungu,jibu linawez kuwa ni kwa sababu kuna kitu Mungu anakuandaa / anakufundisha kivitendo (ikiwa kama umekwisha okoka) Yeye hali akijua maumivu yako,lakini ameruhusu ili akuandae katika utumishi mwema. Na uwe nauhakika kwamba atakuinua tu kwa wakati wake yeye.
Ni kawaida ya Mungu wetu kuwainua watu wasiofaa na kuwapandisha. Mimi ni mmoja kati ya watu ambao BWANA amewainua kutoka kwenye mavumbi.
Hata sasa Bwana amenisaidia sana. Kwa maana sikustahili maisha niishiyo leo,lakini utumishi nilionao leo na mambo mengi tu,sikustahili. Lengo la ujumbe huu ni kukutia moyo kwamba Bwana atakuinua tu mahali ulipo. Katika mazingira yasiyofikirika,mazingira yasiyodhaniwa kuwa utakuja kuolewa au kuao,kujenga,kupata elimu,kupata watoto,kuwa mtumishi n.k hapo ndipo atakapoonekana kwako.
Mara nyingi tunatamani kupanda kimaisha,tunatamani kusogea mbele zaidi,lakini tunashindwa kufikia kwenye mafanikio hayo kwa sababu nyingi tu. Lakini katika hayo yote bado neno la Bwana litasimama vile vile kwamba ni Yeye ambaye mwenye kuinua maskini,na kumpandisha maskini kutoka jaani. Kwa mujibu wa Zab.113:7,ni vyema tukatafakari juu ya mnyonge ni mtu gani hasa? “mnyonge” ni mtu maskini na mtu mwitaji. Huyo ndiye Mungu humwinua na kumpandisha.
Kitu kimoja cha muhimu kujua ni kwamba ni kuendelea tu,kumtazama Bwana katika uweza wake. Yeye anawakati wake wa kukuinua na wala hatakuacha kwa maana wema wake ni mkuu sana. Kama Mungu amewainua wengine,atakuinua na wewe tu. Napenda nikutie moyo tu,
Bwana ni mwema na ni mwaminifu ambaye hataliacha neno lake lipotee lisitimie kwa maana amekuahidi kukuinua kutoka kwenye uhitaji wako. Endelea tu,katika kuomba,upo wakati wa Bwana na utashangaa hayo mambo yatakavyopita,na kubakia historia tu. Mimi ni mmoja wa watu ambao nimebakia na historia tu,kwa maana nimeinuliwa kwa sehemu kubwa sana.
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe.
Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900
What’s app +255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Yorumlar