top of page

UTATEGEMEZWA NA BWANA

Updated: Sep 5, 2022




Kama vile Mungu alivyomuinulia mtumishi wake Eliya Mtishbi,ategemezwe kwa mahitaji yake ya kila siku ndivyo itakavyokuwa kuwa kwako. Wako watu ambao watakao simama na wewe katika  vhali yako unayopitia sasa. Watu hao watatoa chakula,watatoa mavazi,watatoa malazi katika jina la Yesu Kristo,kama asemavyo Bwana siku leo.Inawezekana ukawa hujielewi elewi,huoni msaada wowote. Lakini ninakuambia leo;upo mpango mzuri kwa ajili yako. Maana Mungu wetu anakuwazia mema ( Yeremia 29:11).


Labda tujifunze kwa Eliya Mtishbi. 

Eliya Mtishbi mtu wa Mungu huyu,neno la Bwana lilimjia na kusema kwake,kwamba aende mpaka upande wa mashariki,akajifiche  kwenye kijito cha Kerithi huko Yordani. Naye akafanya vivyo hivyo kama alivyosema Bwana. Akiwa huko kunguru aliandaliwa,amlishe Eliya. Si kana kwamba Eliya alimuandaa Kunguru,bali ni Mungu ndiye aliyemuandaa kunguru kwa ajili ya Eliya ( 1 Wafalme 17:2-6)


Ndege huyu,alikuwa na kazi moja tu,nayo ni kumlisha Eliya Mtishbi mtu wa Mungu.  Bwana Mungu anatufundisha kuwa anaweza kumuandaa mtu yeyote yule,au kuandaa hata ndege,kile ambacho hatukizanii kwamba kiwe msaada kwako,kikutegemeze katika hali yako uliyonayo sasa. Njia za Mungu hazichunguziki hata mara moja,kwa maana pale unapoona hakuna msaada wala njia,Yeye Mungu katika Kristo Yesu huona njia,huona msaada. 


Hakuna angeliweza kufiri kwamba kunguru angeweza kupeleka mkate na nyama kwa Eliya . Kila mmoja wetu anafahamu uroo aliokuwanao kunguru,uroo wa nyama,lakini ndiye aliyetiishwa apeleke nyama na mkate kwa Eliya. Neno la Bwana linakufundisha kwamba vitu vyote vipo mkononi mwa Mungu,na vyote nitiishwa kwa neno la Bwana.  Eliya hakuomba apelekewe msaada,bali Mungu aliandaa kwa ajili yake. 


Na ndivyo itakavyokuwa kwako,Mungu amewaandaa watu kwa ajili yako. Watu si mtu bali watu walioandaliwa watakaotiiishwa kwa ajili ya kukuhudumia,wewe hutawaomba kitu kutoka kwao,bali wao watatoa kitu kwako kwa sababu wametiishwa. Kumbuka; upo mpango wa Mungu kwa ajili yako. Kuna kipindi ambacho kila unaloshika halishikiki,kila unalodanya alifanyiki,na unahisi kuchanganyikiwa lakini mimi napenda leo nikutie moyo,usilie mwamini Mungu nawe utayashinda hayo yote.


Najaribu kuwatazama ndege wa angani ambao hawapandi wala hawavuni lakini ula na kunywa. Ni mpango mzuri wa Mungu huo,wengine wafanikiwe zaidi ili wawasaidie wengine wasiofanikiwa ili nao wafanikiwe kama wao. Bwana Mungu ameruhusu kuwepo hali ya kutegemeana sisi kwa sisi ili tukamilishane,unajua tunahitajiana kila mmoja na ndio maana hata Bwana Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili wawili akiashiria kwamba kazi ya Mungu halifanywi na mmoja tu bali lazima tusaidiane kwa pamoja. 


Ninanaposema watu wa kukutegemeza nina maana ya watu watakaokusapoti kimaombi,kuishauri,kifedha au mali n.k.  Watu ambao yamkini hukumuomba Mungu lakini kwa sababu umekaza kwa Bwana naye amekuuinulia watu. Wewe amini tu kwamba wako watu walio upande wako nao watakunyanyua hapo ulipo. Kusudi ulilobeba ni lazima litimie tu,ndio maana katika kulitimiza hilo anakuletea watu muhimu kwako.


Hivi unajua kwamba,yeyote unayekutana naye katika maisha haikuwa bahati mbaya bali kuna kila kusudi kwa kila unayetukana naye kwenye maisha. Hata kama umefanikiwa kukutana na maskini na ukawa nao katika muda fulani,basi ujue kuna namna ya KiMungu ndani yao na wewe ndio maana wameruhusiwa kwako. Mungu anaweza kukuletea watu maskini,lakini usiwadharau watu hao maana wamebeba hatima ya maisha yako. 


Wengine kati yao watafanyika kama ngazi yako ya kuendea mafanikio. Lakini wengine watakuwa kinyume nawe lakini hao pia unawahitaji sana hao ili wawe pia kama ngazi kwako ya kufanikiwa. Wapo watu watakaosimama nawe katika maisha yako,mimi siwajui lakini amini tu kwamba wapo. Ninazo shuhuda nyingi katika hili maana mimi pia ninao watu walisimama upande wangu. Ikiwa nimefanikiwa katika hili,basi amini nawe utafanikiwa tu.,  Mungu ni mwaminifu sana.


Wito wangu kwako.

Endelea kukaza katika maisha ya wokovu uliyonayo,maana upo karibu na ushindi ni kama vile ambavyo unavyoona timu ya mpira inavyoshambulia zaidi kwa maana vile wanavyoshambulia zaidi ndivyo wanavyokaribia ushindi wa magoli. Hivyo jitahidi sana kungangana na Bwana katika kuutafuta na kuutunza utakatifu wako.


Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900

Namba ya what’s app ni +255 746 446 446


Mchungaji Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page