top of page

BWANA ATAKOMESHA MATESO.

Updated: Sep 5, 2022


Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.” Nahumu 1:9


Ni kitu gani kinachokutesa? Ni wapi unapoteseka? Bwana asema Yeye atakomesha kabisa mateso,hayatainuka mara ya pili,lakini unawaza nini juu yake? Swali hili linakutaka kujua ni nini kinachoendelea kwenye mateso unayoyapitia? Je katika hayo,unamwona Bwana? Au kitika hayo bado unayo nguvu ya kuomba?. Hakuna kipindi kigumu katika maisha kama kipindi cha mateso hasa mateso ya ugonjwa kwenye mwili wako.


Hapo unapokamatwa na udhaifu au ugonjwa ambao kwa kweli kama kuomba uliomba,lakini sasa unawaza nini juu ya Bwana. Watu wengi tukisumbuliwa na mateso ya namna hii,tunajikuta tukimwazia Mungu upumbavu na kuona kwamba Mungu ametusahau,au ametutupa! Hivi ni kweli Mungu anaweza kukusahau? Au anaweza kukutupa? Biblia inasema nini katika hili ? Katika Isaya 49:14-16,biblia inasema Bwana hawezi kukusahau. 

Ikiwa Bwana hawezi kukusahau,basi huna sababu ya kumwazia upumbavu.


Hivyo; Mungu yupo bado upande wako. Yeye amehaidi kwenye neno lake kwamba atakomesha kabisa mateso hii ikiwa na maana kwamba yale unayoyapitia sasa yatakuwa na mwisho wake tu,kwa maana hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho. Hata hayo mateso unayoyaona sasa kuna siku hutayaona kabisa ( Kutoka 14:13-14). Mimi ninaamini kwamba mateso yanakwenda kukomeshwa na Bwana. Ni kuendelea tu kumwomba Mungu kwa imani yote pasipo kukata tamaa!


Tunafahamu kuwa mateso yanaweza kuja kwa sababu nyingi tu. Lakini kwa mujibu wa Neno la Mungu kwenye Nahumu 1:9 tunaambiwa kuwa mateso yatakomeshwa na hatainuka mara ya pili, hii maana yake Bwana hayakomesha mateso/ hatayaruhusu mateso hayo yaendelee kwako kama yalivyokuwa. Lakini jambo la muhimu ni kwamba hayatainuka tena kwa mara ya pili. Ikiwa kama ulikuwa kwenye teso fulani,Bwana hataliruhusu lije tena kwa mara ya pili.


Lakini maneno haya anaambiwa nani? Bila shaka anaambiwa mtu wa Mungu ambaye amemfanya Mungu kuwa ndiye kimbilio kwake. Ikiwa nawe umekuwa na mahusiano mema na Bwana,( umeokoka) basi maneno haya ni ya kwako,ndivyo akuambiavyo Bwana siku ya leo kwamba, Yeye atakwenda kukomesha mateso hayo,na hayatainuka kwa mara ya pili.


Kitu kikubwa cha kujifunza ni kwamba usimwazie upumbavu Mungu katika mateso ya aina yoyote. Jifunze kwa Daudi,pale alipopitishwa kwenye shida,Daudi anasema alimwona Bwana sio shida ( Zab.118:5). Hii inatufundisha kuwa Daudi hakumwazia Bwana ubaya,hata kulalamika katika teso lake kama wengine wafanyavyo leo.


Yeye alimwona Bwana. Usione ukubwa wa tatizo lako bali ona ukubwa wa Mungu wako,kumbuka hilo.


Ikiwa kama umebarikiwa na ujumbe huu,nifahamishe. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900

Whatsapp namba .+255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

留言


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page