top of page

BWANA ANENA NA MUSA NA HARUNI.

Updated: Sep 2, 2022


“BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.” Kutoka 12:1-2

Kipindi ambacho wana wa Israeli wanakaribia kutoka kwenye utumwa wa miaka 430 huko Misri. Bwana alikuwa akisema mara nyingi na Musa na Haruni na kuwatuma wamwendee


Farao na kumtaka Farao awape ruhusa watu wa Mungu watoke,na kumtumikia Mungu. Hata hivyo Farao alikataa mara nyingi maana moyo wake ulikuwa ni moyo mgumu. Farao na watu wake walipigwa kwa mapigo makuu kumi,mapigo hayo yote ni miungu yao ndio iliyokuwa ikipigwa,kwa maana walikuwa ni waabudu miungu mbali mbali.


Baada ya pigo la tisa,hapo sasa BWANA anatoa maelekezo mapya na kusema kwamba“… Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.“ Kutoka 11:1


Biblia inatuambia katika Kutoka 12:1-2 ( mistari iliyopo hapo juu). “BWANA akasema na Musa na Haruni katika nchi ya Misri…” Jambo kubwa la kwanza kujifunza hapo ni;


01. BWANA husema na mtu mahali popote.


Musa na Haruni hawakuwa Hekaluni,au Yerusalemu bali walikuwa “ Misri” lakini ingawa walikuwa Misri bado BWANA aliweza kunena nao. Hii inaonesha kuwa Yeye ni Mungu wa namna gani,ni Mungu asiyezuiliwa na mipaka tuliyonayo,Yeye yupo kila mahali,yupo Yerusalemu hata Misri pia yupo kwa watu wake. Hata sasa unaweza ukawa popote pale,lakini BWANA anapohitaji kusema nawe ujue lazima atasema nawe tu kwa njia yoyote atakayo Yeye.


Hata ukiwa Misri bado( dhambini),ujue Yeye Mungu hafungwi na Misri atasema na wewe tu. Kwani kikowapi! Kwa habari ya Kornelio? ( Matendo 10:1-5) Ingawa alikuwa ni mtu anajitoa sana kwa Mungu na ni mtu wa sala,lakini bado alikuwa Misri ( hajaokoka),Mungu akasema naye huko huko kwenye Misri yake ( kwenye udini wake) naye akaokoka.


02. Wokovu,mwanzo wa maisha mapya.


Biblia inasema “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu” bila shaka unajua kwamba, kitendo cha waisraeli kutoka Misri,utumwani ni kitendo kile kile cha kutolewa kutoka utumwani,dhambini kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ( Wakolosai 1:13-14).


Waisraeli walikuwa na karenda yao ya kawaida yenye masiku na miaka. Lakini pale Mungu alipokuwa akiwatoa aliwaambia wataanza upya,mwezi ule utakuwa ni mwezi wa kwanza kwao.

Katika kipindi kile ulikuwa ni mwezi wa nne mwezi wa Abibu, ndio maana Wayahudi wa leo wana kalenda mbili ( kalenda ya kiserikali na kalenda ya kidini). Katika kalenda ya kidini,mwezi wa nne ni mwezi wa kwanza kwao katika mwaka,ni mwenzi wa “Pasaka” ambapo dunia nzima tunaadhimisha pasaka katika mwezi huo huo. Hii ina maana gani? Bila shaka “ Pasaka ni kutoka, ukombozi”. Hivyo,kila aliyetoka / aliyeokolewa ni kiumbe kipya,ya kale yamepita ( 2 Wakorintho 5:17)


Katika yote hayo,BWANA Mungu anazungumza na watu wake hata sasa katika mazingira ya aina mbali mbali. Wapo watu ambao husikia sauti ya BWANA,lakini wengi hatuwezi kusikia sauti,lakini hata hivyo BWANA ana njia nyingi za kusema nawe katika mazingira ya aina yoyote. Musa aliweza kunena na Misri,hii ina maana kwamba mazingira hayakumweza Musa. Kwa maana katika yote,bado kulikuwa na mazungumzo kati yake BWANA na Musa labda Musa naye alikuwa akisema kitu.


Leo hii,ikiwa utakuwa na mazungumzo na Bwana, mazungumzo hayo huitwa ni maombi. Lakini Je ni kweli ukiwa katika Misri yako,waweza kuisikia sauti ya BWANA, au Je waweza kuomba? Kwa maana Misri ya leo yaweza ikawa ni sehemu ya mateso ( labda ikiwa ni sehemu ambayo kweli kabisa kuna hali ngumu na ya uchungu) Je waweza kujikaza na kuisikia sauti ya BWANA katika wakati mgumu wa maisha yako?


Ukweli ni kwamba wengi hawawezi kuomba,au kuisikia sauti ya BWANA kwa maana katika kipindi kigumu,watu hawaombi na wakiomba wengi hulalamika na kufanya kushindwa kuisikia sauti ya BWANA kikamilifu.


Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,


Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900


What’s app namba ni +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Комментарии


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page