BAHARI YA CHUMVI / DEAD SEA
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 17, 2019
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Ukifabahatika kuzuru Israeli,basi bila shaka utapekwe kwenye eneo la maajabu liitwalo “ bahari ya chumvi” naliita eneo la ajabu kwa sababu ya wa bahari mfu. “ AHAVA ” moja ya kampuni maarufu inayouza bidhaa zinazotokana na maji na matope ya bahari ya chumvi. Huu ni mfano wa kuonesha kwamba matumizi ya bahari ya chumvi yanakuwa kila siku,kwa maajabu yake.
Miaka fulani nilipata neema kutembelea bahari hii,nami nikashangaa kidogo kuona mtu akielea juu ya maji pale alipojilaza bila kuzama kwa sababu ya uzito wa maji yake yenye chumvi kubwa. Utafikiri ni utani fulani lakini ndio maajabu ya Mungu mwenyewe.
Kwa mara ya kwanza biblia inalitaja eneo hili katika zama za Abramu,zamani sana hata kabla ya Abramu kuwa Ibrahimu. Kilikuwa ni kipindi cha vita kati ya wafalme wa Shinari na wafalme wa Sodoma,na wote hawa walikutana kwenye bonde la Sidimu ndio bahari ya chumvi ( Mwanzo 14:3)
Hapo mwanzo lilikuwa ni bonde kubwa liitwalo “Sidimu” na ilikuwa ni moja ya mpaka kati ya mto Yordani na maeneo mengine ( Hesabu 34:11-12). Ni eneo muhimu sana unapozungumzia mto Yordani. Hivyo bahari ya chumvi imebeba sifa zifuatazo;
Ni ya kale sana ( Mwanzo 14:3)
Ipo sehemu ya chini zaidi duniani ,ina usawa wa maji yake mita 400 chini ya usawa wa bahari.
Hakuna kiumbe hai kinachoishi mfano wa samaki ( kwa sababu ya chumvi kubwa)
Maji na matope yake hutengenezewa dawa. ( watafiti wamebuni dawa mbali mbali za ngozi )
Ni kitovu cha kibiashara kwa leo.
Ina urefu wa Kilometa 75,upana kilometa 15. ( Hivyo ni kubwa kiasi chake)
Kwenye kipindi cha Yoshua iliitwa mara moja kuwa ni bahari ya Araba ( Yoshua 3:16). Yapo mengi kuhusu “ bahari ya chumvi ” lakini hayo machache yanakutosha. Kwa msaada zaidi piga kwa +255 683 877 900
Whats app namba+255 746 446 446 .
Mch.G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários