AMEFUFUKA KWELI KWELI.
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 10, 2018
- 2 min read
Shalom…
Kwa ufupi tu.
Kuna mambo yaliyojificha mengi ambayo baadhi yake nina uhakika huyajui ingawa inawezekana ukawa unayasoma kila siku pasipo kuyaelewa. Imenilazimu leo kuandika matukio saba baada ya Yesu kufufuka pale msalabani. Matukio haya ni namna alivyojidhihilisha kwa wanafunzi wake mbali mbali. Lengo kuu la ujumbe wa leo ni kukupatia maandiko na sehemu pamoja na siku ya matukio ya kujidhihilisha kwa Bwana. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;
Kaburi lilikuwa wazi. ( Huko Jerusalemu siku ya Jumapili) – Soma Mathayo 28:1-10,Marko 16:1-8,Luka 24:1-12 na Yohn.20:1-10
Hili ndilo tukio la kwanza kubwa lililowaacha wayahudi midomo wazi. Wale waliokuwa hawamwamini ilibidi watafute kujua kweli,Hawakujua Yesu ni Mungu pia.Kumbuka ; Yesu hakushikwa na uchungu wa mauti kwa sababu mauti haikumweza ( Matendo 2:24)
Mariamu Magdalena anakutana na Yesu kwenye bustani. ( Huko Jerusalemu siku ya Jumapili) – Marko 16:9-11,Yohn.20:11-18
Huyu ndiye mwanamke wa kwanza kuhubiri injili ya ufufuo. Watu wanadhani wanawake hawakuwa na nafasi kabisa kwenye huduma ya Bwana,si kweli kwa maana Yesu namtuma mtu wa kwanza kwenda kutangaza habari njema za wokovu,na mtu huyo hakuwa mwanaume bali mwanamke.
Yesu akiwatokea watu wawili walioshika njia kwenda Emausi. ( Siku ya Jumapili) – Marko 16:12-13,Luka 24:13-35.
Baada ya tukio zima la kusulubiwa Yesu,jamii ya waaminio walikuwa wakiogopa hofu ya wayahudi na maisha yao. Ni kweli waliendelea kuamini lakini katika hali ya hofu kubwa. Yesu alilijua hili,hakajidhihirisha kwao katika njia na wakati mbali mbali kwa lengo la kuonesha ukamilifu wa unabii kwamba mwana wa Adamu atateswa,atakufa na siku ya tatu atafufuka katika wafu,na kweli yametimia sasa.
Yesu akiwatokea wanafunzi 11 huko Jerusalemu, Jumapili (Marko 16:14,Yohn.20:19)
Wiki moja baadae,Yesu akiwatokea tena wanafunzi wake 11 ,Jerusalemu ( Yohn.20:26-31)
Wiki moja baade,Yesu akiwatokea wale wanafunzi 7,Tiberia Jerusalemu ( Yohn. 21:1-25)
Baada ya siku 40,kwenye mlima wa mizeituni ( Matendo 1:1-12,Mathayo 28:16-20)
– hapa ndipo alipotoa agizo kuu,linaitwa agizo kuu la Bwana la kwenda kufawafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wakibatizwa pia kwa Jina la Baba,na Mwana na Roho mtakatifu.
Ikiwa fundisho hili limekubariki,basi ningependa kusikia kutoka kwako kwa kuniandikia msg au kunipigia kwa namba zangu zilizopo hapo juu. Pia kwa msaada zaidi pamoja na maombezi,waweza kunipigia sasa.
Kwa mawasiliano na maombezi +255 683 877 900
Na mch. Gasper Madumla.
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Commenti