top of page

AINA TATU ZA IBADA

Updated: Sep 2, 2022



Awali ya yote tufahamu kwamba Kila mmoja wetu ameumbwa ili “kuabudu”. Na ndio maana kama mtu hataweza kumwabudu Mungu basi ujue atamwamudu shetani kwa maana hakuna mtu anayeweza kuishi bila ibada. Ibada ni jambo ambalo Kila mwanadamu amepewa.

Hivyo neno “ibada” limetokana na neno la kiingereza “worship” lenye maana ya kutukuza , kuheshimu pamoja na hali ya kuonesha kumtegemea Mungu. Asili ya kuabudu ni Mungu mwenyewe ( Kila mtu aliumbwa ili amwabudu Mungu pekee)


Tangu hapo awali Adam na Hawa walikuwa wakimwabudu Mungu kwa maana walikuwa na ushirika wa kiroho mkubwa. Lakini dhambi iliwavuruga na tangu hapo ibada halisi ilipotea ndani ya moyo wa mwanadamu. Watu waliishi kiholela olela, lakini kizazi cha Sethi kikarudisha “ibada ya maombi ” Mwanzo 4:26


Hata hivyo, dhambi iliendelea kumfanya mwanadamu kugeukia katika aina mbali mbali za ibada. Na hapo kukatengenezeka aina kubwa tatu za ibada ambazo;


  1. Ibada kwa Mungu aliye hai.

  2. Ibada kwa miungu ya jadi,mizimu, matambiko na mashetani.

  3. Ibada kwa mwanadamu,vitu,fedha na mali


Katika ibada hizo tatu,ndizo zinazofanyika chini ya jua hili. Ukijitafakari wewe mwenyewe utagundua labda kuna moja ya ibada katika hizo unaifanya. Biblia inaeleza vizuri sana kuhusu aina hizo tatu za ibada.Katika ibada hizo tatu,ndizo zinazofanyika chini ya jua hili. 


1.Ibada kwa Mungu aliye hai. ( Mwanzo 12:7-8,Matendo 2:42)


Kila mtu mwenye hofu ya Mungu alifanya ibada kwa Mungu wa kweli. Suala la kumfanyia Bwana Ibada linahusisha na hali ya kuwa na “hofu ya Mungu” au roho ya kicho. Hivyo ibada ya kweli hufanyika katika roho na kweli ( Yoh. 4:23-24).

Tunaposema “ibada katika roho na kweli” tuna maana ya ibada itokayo moyoni,hivyo kinachohusishwa zaidi sio akili pekee za mwanadamu Bali Roho mtakatifu pamoja na roho ya anayeabudu. Roho mtakatifu ndiye hasa mwenye kuongoza ibada halisi,ndio maana ikiwa kama unataka umfanyie Bwana ibada halisi huna budi kumwomba sana Roho mtakatifu akuongoze.


2. Ibada kwa miungu.( 1 Wafalme 18:26, Yoshua 24:2 Mathayo 4:9)


miungu yote hutafuta sana kuabudiwa. Hata shetani naye hutafuta sana aabudiwe. Kuna wakati mwanadamu anapoona mambo yake yamechelewa kufika au kuyapata,wengi hugeuka katika aina hii ya pili ya ibada ya machukizo kwa kuomba mizimu au kukimbilia kwa waganga wa tunguli. Kwa kweli tumeshuhudia ibada ya mizimu ikiendelea mpaka leo kwa maana watu wafanyao ibada hizi, wamefungwa nao wamejikuta wakiendelea kuabudu mizimu, waganga,mila na desturi za kale zilizo machukizo makubwa kwa Mungu.


3. Ibada kwa mwanadamu,vitu, fedha au Mali. ( Warumi 1:21-23)


Kuna watu wanaabudu watu na wengine wanaabudu fedha na mali yaani fedha na mali zimekuwa ni miungu kwao. Katika aina hii ya tatu ya ibada mbaya inayoendelea kufanyika kwa kasi sana chini ya jua,tumeona vile ambavyo adui ibilisi akiwapa maarifa watu wake na kuwafanya miungu watu.


Hivi unajua kuna watu ambao hujiita wao ni Mungu,na papo hapo watu wengine huinama mbele zao kana kwamba mtu mmoja ainamavyo mbele za Bwana Mungu . Tena kwa hila,adui anawatumia hata watu ambao huitwa watumishi wa Mungu.


Ndio maana unaweza ukamwona mtumishi akijiita Mungu,wakati mwingine kuwanyanyasa watu kwa kuwatisha! Katika aina tatu hizo ni vyema ukatafakari upo wapi wewe? Ni vyema ukabaki katika aina ya kwanza ya ibada,ambayo ya kuendelea kumwabudu Mungu peke yake.


Kwa msaada zaidi na maombezi piga  +255 683 877 900.

What’s app number ni +255 746 446 446


Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page