top of page

AGANO LA KALE ~ 03/tamati

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Hata hivyo,vitabu mashairi vinasisimua kwa ujumbe uliobebwa,utafikiri ni unabii fulani ukielezwa. Robo tatu ya agano la kale ni mashairi ( vitabu vitano),sehemu hii,tunafundishwa mengi,mfano;

  1. Kitabu cha AYUBU kinajibu swali la msingi “ kwa nini mwenye haki anaweza kuteseka“

  2. Kitabu cha ZABURI ni kitabu cha maombi na sifa mbele za Mungu.

  3. Kitabu cha MITHALI,hekima ndio inayosemwa inayotupasa kuijua na namna ya kutembea nayo.

  4. Kitabu cha MHUBIRI,Sulemani anajaribu kueleza kutafuta mali bila Mungu ni ubatili mtu na kujilisha upepo,na kutoa njia iliyo bora ya kumwendea Mungu.

  5. Kitabu cha WIMBO ULIO BORA,kinatoa picha ya ajabu penzi ambalo mwanadamu analokuwa nalo,kuonesha kama vile unavyoweza kumpenda mpenzi,ukampa muda wako,pesa,moyo,akili,n.k ndivyo hivyo hivyo, vielekezwe kwa Mungu.

Vitabu vya manabii;

Vitabu hivi 17 vya manabii kutoka Isaya hadi Malaki, vimeandikwa na waandishi mbalimbali waliovuviwa na Roho mtakatifu,na ndio maana ni ngumu kuelewa ujumbe uliopo kama hukuongozwa na Roho mtakatifu. Manabii walikuwa na kazi ya kuwapa watu ujumbe kile alichosema Mungu, kwa hiyo “ kuhani husema na watu kupeleka kwa Mungu,bali nabii husema na Mungu kwa ajili ya watu” hii ni sawa na kusema Mungu alikuwa akitumia vinywa vya manabii kusema na watu ( lakini makuhani hupeleka kwa Mungu yale yote ya watu). “ a priest speaks for man to God,but a prophet speaks for God to man”

Kazi ya manabii ilikuwa ni kazi kubwa mno,kwa maana ni kama kinywa cha Mungu. Kwa hiyo chochote wakisemacho ni lazima kitimie,na lazima Neno liwe la Mungu kweli. Manabii wa kubwa na wale wadogo (utofauti huo ni kulingana na ukubwa wa maandiko),tunaweza kuwagawa katika makundi matano kwa mujibu wa kazi zao;

  1. Kundi la kwanza; Kundi la Eliya “ Maonyo ya kwanza ” Kwenda Edomu – Obadia,Kwenda Israeli – Eliya na Elisha,Kwenda Yuda – Yoeli.

  2. Kundi la pili ; Kundi la Isaya “ maonyo ya mwisho” Kwenda Ashuru – Yona,Kwenda Israeli-Hosea na Amosi,Kwenda Yuda-Isaya na Mika.

  3. Kundi la tatu;Kundi la Yeremia“ hukumu“Kwenda Ashuru-Nahumu,Kwenda Yuda-Habakuki,Sefania,Yeremia,maombolezo.( Yerusalemu na hekalu lilikuwa limebomolewa tayari)

  4. Kundi la nne;Kundi la utumwa “Tumaini/hope” Kwenda kwenye mabaki ya uhamisho wa babeli – Ezekieli na Danieli

  5. Kundi la tano; urejesho “kutia moyo” Kwenda kwa watu wote waliorejea kutoka utumwani babeli – Hagai,Zekaria,na Malaki.

Summary ya vitabu vyote na kusudi lake.

  1. Mwanzo- Mwanzo wa kila kitu,na mgawanyo wa baraka.

  2. Kutoka-Ukombozi,kutoka.

  3. Walawi-taratibu za ibada / kuabudu

  4. Hesabu- Nidhamu na mpango wa nchi ya ahadi.

  5. Kumbukumbu la torati – maelekezo kwa kizazi cha pili,kuhusu maisha ya imani kwenye nchi ya ahadi.

  6. Yoshua-ushindi kwenye nchi ya ahadi/ Kanaani.

  7. Waamuzi- kuzunguka dhambini na wokovu.

  8. Ruthu- Yeye asiyekuwa na kitu,kuzidishiwa ( Naomi)

  9. 1&2 Samweli – utii & unyenyekevu “ Exalted & humble

  10. 1&2 Wafalme- Kukengeuka kwa taifa la Mungu.

  11. 1&2 Nyakati-Kutiwa moyo.

  12. Ezra- Kujengwa kwa hekalu.

  13. Nehemia- kujenga tena ukuta wa Yerusalemu. Na kuwafundisha sheria ya Mungu.

  14. Estar-Ukombozi kupitia binti wa Kiyahudi.

  15. Ayubu-Mateso ya mwenye haki.

  16. Zaburi-Maombi na sifa kwa Mungu

  17. Mithali-Hekima

  18. Mhubiri- kila kitu ni ubatili bila Mungu.

  19. Wimbo bora-mapenzi

  20. Isaya-maono makubwa Yuda na Yerusalemu.

  21. Yeremia- Agano jipya la Mungu (Baada ya kulivunja agano la kale)

  22. Maombolezo- Mungu anayependa huruma/ huruma yake Bwana.

  23. Ezekiel – Uzima kutoka kwa Mungu/Neno la Mungu lina uhai ndani yake

  24. Daniel-Mungu anatawala juu ya kila falme.

  25. Hosea-Huruma ya Mungu

  26. Yoeli-Siku ya hukumu ya Bwana imekaribia

  27. Amosi-Haki ya Mungu

  28. Obadia-Kisasi cha Mungu

  29. Yona- Mungu kuzidisha uvumilivu wake kwa ,ili watubu.

  30. Mika- Haki y Mungu na huruma yake.

  31. Nahumu-Mungu uhukumu kwa vyote.

  32. Habakuki- Faraja ya Mungu /God’s comfort

  33. Sefania-Hukumu ya Mungu

  34. Hagai- Kipaumbele cha Mungu

  35. Zekaria-ujenzi wa hekalu

  36. Malaki-Muheshimu Mungu.

Zingatia;

Agano la kale linasomwa kwa jicho la agano jipya,kwa maana ni kivuli cha agano jipya. Katika bilia yote (agano la kale na jipya) linamzungumzia Yesu kwenye kiini cha “ukombozi“,kila simulizi,imeandikwa kwa sababu ya “Kutufundisha,kutuongoza,kutuonya na kutuadabisha“. Pili; Mungu amejifunua katika nyakati tofauti tofauti,katika neno lake. Hivyo,haipaswi kuacha kusoma agano la kale kwa maana Mungu amejifunua huko pia.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp namba +255 746 446 446

Mch. G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page