top of page

AGANO LA KALE ~ 02

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Baada ya vitabu vya sheria vitano,vitabu vya historia vinafuata. Kwa sehemu kubwa tunaona Israeli akishindwa kutii,na kuangukia dhambini kulikompelekea kwenye “uhamisho wa Babeli” ( exile). Hata hivyo kwa neema ya Mungu, aliwarudisha watu wake. Vitabu hivi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu;

  1. Mungu akitawala mwenyewe – Wakati Mungu mwenyewe anaiongoza nchi,serikali hiyo huitwa“theocracy“. Mfano wa vitabu vilivyoendeshwa na serikali hii ni Yoshua,Waamuzi,Ruth,1 Samweli 1-7.

  2. Wafalme wakiongoza – Kipindi wafalme wakiongoza/wakitawala nchi,serikali ya na namna hiyo huitwa “ Monarchy” vitabu sita vinatawaliwa na serikali ya namna hii, Vitabu vya Samweli,Wafalme na Mambo ya nyakati.

  3. Urejesho – Wakati Wayahudi wanarudi kutoka katoka Baberi kwenda Yerusalemu, huitwa ni “ Restoration” Vitabu kama Ezra,Nehemiha na Esta.

Katika vitabu hivi,ni vyema nikachambua kuhusu wafalme wa kaskazini – Israeli na wafalme wa kusini – Yuda,ili kusudi kuongeza ufahamu kidogo. Hivyo,Kipindi cha Samweli kama mwamuzi wa mwisho wa Israeli, Waisraeli walidai watawaliwe na wafalme. Walitamani wafalme, wakidhani wataenda vyema zaidi ya waamuzi,pasipo kujua kwamba kile kinachowafanya watende dhambi haikuwa kwa sababu ya utawala bali ni utii wao uliopungua mbele ze Mungu.

Hata hivyo,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,Samweli akampaka mafuta Sauli awe mfalme wa kwanza. Sauli mfalme alianza vyema lakini alimalizia vibaya kwa sababu hakutii kile alichoambiwa na Bwana. Hata hivyo Sauli aliendelea kuwa mfalme kama kwa miaka 40 hivi,lakini Mungu akamwambia Samweli akampake mafuta Daudi,Sauli akawa na wivu mkubwa sana na mara nyingi akitafuta kumwua Daudi. Baadae Daudi alikuwa mfalme, naye akatawala vyema, ingawa utawala wake ulikuwa umegubikwa na changamoto nyingi,ikiwemo dhambi ilikuwa ni changamoto yake. Baada ya Daudi alifuata mfalme Sulemani.

Sasa, baada ya kifo cha cha Sulemani katika 931 KK,Israeli ikagawanyika katika falme mbili

  1. Ufalme wa kaskazini – Israeli.

Kila mfalme wa kaskazini alikuwa mbaya,yaani alitawala vibaya kwa kufanya dhambi juu ya dhambi. Wafalme wa kaskazini waliotawala walikuwa ni “ Yerebohamu,Nadab,Baasha,Elah,Zimri,Omri,Ahabu na Yezebeli mkewe,Ahazia,Yoramu,Yehu,Yehoahaz,Yehoashi,Yerobohamu II,Zakaria,Shallum,Menahem,Pekahiah,Pekah,Hosea” ~ Hawa wote walitawala katika nyakati tofauti tofauti wakiabudu sanamu na miungu ya kigeni.

Manabii wa ufalme wa ufalme wa kaskazini.

Kwa pendo la Mungu, hakuwaacha wapotee kwani aliwapelekea manabii kwamba wageuke. Nabii kama “ Eliya,Elisha,Yehu( kutoka Yuda),Mika,Amosi,Hosea,Yona”. Hata hivyo haikusaidia kabisa,hivyo MUNGU akaruhusu waangukie kwenye mikono ya Waashuru na kamwe hawakurudi tena,( Walivamiwa/kuharibiwa na kutekwa nao hawakurudi tena)

  1. Ufalme wa kusini – Yuda.

Ufalme huu una wafalme wabaya na wazuri pia. Mungu alituma manabii ili Yuda itubu na kutejea kwa Bwana. Wafalme kama “ Rehoboamu,Abiya,Yoramu,Ahazia,Athaliah,Yoashi,Amaziah,Uzia,Yotham,Ahazi,Manase,Amon,Yehoahaz,Eliakimu,Yehoachin,Zedekia” hawa walikuwa ni wabaya,ingawa Yoashi,Amaziah,Uzia walikuwa kidogo wamefanya mazuri. Lakini wafalme waliofanya mazuri ni kama “ Asa,Yehoshafati,Hezekia na Yosia” . Hata hivyo,ufalme huu pia uliangukia kwenye mikono ya Wababeli,Wayahudi wakapelekwa Babeli ( uhamisho wa Babeli).

  1. Urejesho ( Ezra na Nehemia)

Mungu aliwarejesha Wayahudi Yerusalemu. Urejesho wao ulikuwa katika hatua tatu tofauti tofauti, kama ifuatavyo;

  1. Ezra 1-6,Kurejea kwa mara ya kwanza ( 538/537 KK) chini ya utawala wa Zerubaleli. ~ Kama vile Yeremia alivyotabiri,baada ya miaka 70 watarejea Yerusalemu ( Yeremia 25:11-12). Makadirio ka Wayahudi 50,000 hivi waliweza kurejea ( Ezra 2:64-67) nao wakaanza kazi ya kujenga tena Hekalu. Katika 520KK,Mungu alituma manabii wawili Hagai na Zekaria kwa ajili ya kuwatia moyo watu kukamilisha kazi hiyo.

  2. Ezra 7-10,Kurejea kwa mara ya pili (458KK)chini ya utawala wa Ezra. ~ Ezra alikuwa ni kuhani ambaye aliyefundisha sheria ya Mungu kwa watu,na kuwaongoza katika harakati mpya za kiroho.

  3. Nehemia 1-13,Kurejea kwa mara ya tatu(445KK) chini ya Nehemia ~ Nehemia aliongoza ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu. Pia kwa Ezra akawarejesha watu kwa Mungu. Malaki ambaye ndiye nabii wa mwisho kwenye agano la kale,aliishi kwenye kipindi hiki.

Muktasari wa vitabu vya historia.

  1. Yoshua kinahusu haswa kuingia(conquest) kwenye nchi ya ahadi.

  2. Waamuzi kinahusu mzunguko wa matukio ya makosa/dhambi ( sin cycle) ikawapeleka kupata adhabu,walipotubu,waamuzi wakaja.

  3. Samweli,Wafalme, na Nyakati,waislaeli wakihitaji utawala wa kifalme,Sauli akaanza,Daudi,kisha Sulemani akafuatia.

  4. Ezra na Nehemia kuhusu urejesho wa Wayahudi kwenda Yerusalemu

  5. Esta ni ukombozi kupitia mwanamke Esta,kukomboa Wayahudi kutoka kuangamizwa na watesi wao.

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp namba +255 746 446 446

Mch. G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page