top of page

AGANO LA KALE ~ 01

Bwana Yesu asifiwe…

“Agano la kale / Old testament”

Kwa ufupi,

Agano la kale lana vitabu 39 vilivyoandikwa kama miaka 1000+ katikati ya 1440 KK ( Kabla ya Kristo) na 400 KK. Agano liliandikwa kwa lugha ya kihebrania ( sehemu ndogo sana kwa lugha ya Kiaramu),watu maalumu tofauti tofauti walitumiwa na Mungu kuandika na kumalizika kwa kazi ya uandishi kama miaka 400 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.

  1. Lakini kwa nini tunasoma agano la kale wakati kuna agano jipya?

Hili ndilo swali la msingi sana. Kwa maana kuna haja gani kutumia muda mwingi katika agano la kale wakati agano jipya lipo sasa. Kwa mujibu wa swali hili,limewafanya watu wengine kuacha kusoma kabisa agano la kale, wengine wamejikuta wakisoma na kuyaona mambo wayasomayo yamepitwa na wakati,

hivyo hawawezi kuyachukua. Na kundi jingine la watu,husema “ sisi hatupo tena chini ya sheria,sasa agano la kale lenye sheria la nini kwetu? Sisi tumeokolewa tayari!!”. Katika mitazamo hiyo,kuna kitu kimekosekana,nacho ni kwamba hatujui vizuri kwa nini tunasoma agano la kale wakati huu? Hivyo kuna sababu kubwa mbili zinazotufanya kusoma agano la kale, nazo ni;

01. Agano la kale linamzungumzia Yesu. ( Luka 24:27,44,Yoh.5:46)

Ukweli ni kwamba, agano la kale limeandika habari za Kristo kutoka Musa hadi manabii wote. Na yote yaliyoandikiwa kuhusu Yeye,ni lazima yatimie yote. Kwa sababu hiyo hiyo,wale wote waliomwamini masihi Kristo, ingawa hawakumwona walihesabiwa haki/ waliokoka.[ Mfano mzuri ni kutoka kwa Ibrahimu baba wa imani,mtu ambaye aliamini tu,akahesabiwa haki. ( Mwanzo 15:6). ] – Tena, kuna nabii kama 300 katika agano la kale zinazo muhusu Yesu,ambazo zimetimilika katika agano jipya.

Biblia inaendelea kusema “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.” Waebrania 13:8 maana ya neno “ jana” ni muda wa kuanzia agano la kale,yaani tangu enzi hizo. Neno hili “jana”halina maana siku moja iliyopita kutoka leo. Hivyo tangu agano la kale, Yesu alikuwepo na ndiye aliyeandikiwa habari zake hata sasa,na hata milele. Kwa sababu Yeye Kristo ndie mhusika mkuu ( main character),hapo hatuna budi kujifunza kutoka kwake.

02. Agano la kale linazungumza ukombozi kupitia Kristo kama lilivyo agano jipya. ( Mwanzo 3:15 )

Wokovu ni mpango wa Mungu kwa wanadamu wote watakao mwamini Kristo na kumpokea. Mpango huu,haukuanzia kwenye agano jipya, bali kwenye agano la kale pale mwanadamu alipoanguka dhambini. Ahadi ya ukombozi kwa mara ya kwanza inatajwa katika Mwanzo 3:15. Lakini pili,biblia inasema kila andiko la Mungu lina pumzi…( 2 Timotheyo 3:16). Hii ikiwa na maana hata agano la kale ni moja ya maandiko ya Bwana yenye pumzi yake. Kwa sababu hiyo,ni lazima tusome agano la kale

03. Kufundisha na kutupa tumaini.( Warumi 15:4)

Kila simulizi iloyoandikwa imebeba ujumbe maalumu kwa ajili yako,kukufundisha. Mfano; Ikiwa mtu amekosea basi ujue namna gani usije ukakosea kama huyo. La! Ikiwa mtu alifanya vyema,basi ujitahidi kwa msaada wake Mungu ufikie kiwango kama cha mtu huyo. Lakini zaidi sana,agano la kale linatufundisha imani,ili tupate tumaini leo. Kwa maana Bwana amejifunua kwa nyakati tofauti tofauti kwa kusudi tuweze kujifunza kwa saburi.

Agano la kale, unalisomaje?

Agano la kale linasomwa kwa jicho la agano jipya. Kwa maana kile kilichoandikwa kimeandikwa kama kivuli cha agano jipya ( Waebrania 10:1a). Hivyo,msomaji ni lazima amuhusishe “Roho mtakatifu” Yeye awezaye kukufunulia jambo hilo katika agano jipya. Lakini ikiwa kama utasoma agano la kale kama lilivyo,litakusumbua!

Wakati tunaposoma agano la kale, ndipo tunapoelewa vyema agano jipya.

Kwa kuwa agano la kale limejengwa kwenye msingi wa Yesu (The Old Testament so clearly points to Jesus),sasa tunapolielewa ni sawa na kuanza kuelewa agano jipya. Lakini ikiwa kama utalitupilia mbali,basi ni vigumu sana kumwelewa Yesu na agano jipya kwa ujumla wake. Hii ni sawa na mwanafunzi anayetaka kujua kuhesabu na gafla akaanzia kujifunza kuhesabu kuanzia namba 11 na kuendelea huku namba 0,1 mpaka 10 hazijui!!!

  1. Vitabu vya sheria

Vitabu hivi vina majina mbali mbali,wakati mwingine huitwa “Sheria” au “ Pentateuk/ The Pentateuch/ in latin,au “ Torati” au “vitabu vya Musa“. Musa ndiye mwandishi wa vitabu hivi,naye aliishi miaka 120 ambayo miaka yake imegawanywa katika sehemu tatu

  1. Miaka 40 akiwa kwa Farao katika ukuaji wake.

  2. Miaka 40 aliitumia huko Midiani,kwa Yethro mkewe kwa maana alimkimbia Farao baada ya kumwua Mmisri

  3. Miaka 40 alipokuwa amerejea Misri,kuwakomboa Israeli kutoka utumwa Misri. Musa alipokuwa anatumwa na Bwana alipata miaka 80 ,na Haruni ndugu yake alikuwa na miaka 83.

Katika muktasari wa vitabu hivi vitano ( Mwanzo, Kutoka,Mambo ya walawi,Hesabu na Kumb.la Torati),tunajifunza kwamba, kila kitabu kilikuwa na kusudi lake. / Yaani kiliandikwa kwa kuzungumzia nini hasa. Kila kimoja kilikuwa na lengo moja kubwa;

01. Mwanzo – kinahusu “mwanzo wa kila kitu” kutoka uumbaji na namna Mungu alivyojichagulia taifa lake ( Israeli)

02.Kutoka – kinahusu “ ukombozi / Redemption or rescue” kuanzia kwa Wayahudi utumwani Misri.

03.Walawi – kinahusu “ taratibu za ibada / kuabudu / worship” Kitabu kinafunua namna gani Waisraeli wanapaswa wanaweza kuwa na ushirika na Mungu.

04.Hesabu – kinahusu “ kushindwa / failure” miaka 40 ya maajabu Mungu aliyoitumia kwa kuwafanya angalau waamini,lakini hata hivyo hawakuamini.

05.Kumbukumbu la torati – kinahusu “ maandalizi / preparation” pamoja na Musa,Musa akijaribu sana kurudia sheria kwa kizazi kitakachoingia kwenye nchi ya ahadi. Musa akieleza sana tahadhari watakazozipata kama Waisraeli wasipotii neno la Mungu.

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp namba +255 746 446 446

Mch. G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page