top of page

ADUI WA KWANZA WA IMANI.

Na Mch.G.Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Imani ina maadui wengi. Maadui wengine hutokana na shetani na wengine hutokana na mwenendo wako  wa kila siku. Naonelea nimwache kidogo shetani ambaye yeye naye ndiye adui mkubwa wa imani,lakini nijikite na maadui wa upande wako mwenyewe. Tumwangalie adui namba moja wa imani naye si mwingine ni “roho ya mazoea”.

Huyu ndiye adui mkubwa na wa kwanza katika imani yako,kwa maana kama hutaweza kumshinda basi ujue hakika utapishana na muujiza wako. Hivi unajua wengi leo,wamekula hasara kwa sababu ya kuzoelea wokovu! tena bahati mbaya hata watumishi wa Mungu wameshindwa kukutana na Mungu kwa sababu ya roho ya mazoea.

Lakini ni vyema kujiuuliza kwa nini roho ya mazoea? imetoka wapi? nini asili yake?. Moja ya sababu inayofanya mtu kutembea katika roho hii ni tabia ya kiburi ( kujiona unajua kila kitu,au kuona kila kinachofundishwa ulishawahi kujifunza). Baadhi ya athari au madhara machache ya adui huyu ni kama ifuatavyo;

  1. Kuzuia kuvuka kiroho

Kawaida kabisa,kama Bwana amekusudia kukuvusha basi atakupelekea Neno la kukuvusha eneo fulani. Neno lake laweza kukujia kwa njia tofauti tofauti. Moja ya njia ambayo Bwana hutumia neno la kukuinua au kukuvusha ni kutumia vinywa vya watumishi wake. Sasa roho ya mazoea,inachofanya ni kuanza kumjadili huyo mnenaje,na kupima kila kitu. Na hapo ndipo mahali ambapo huwezi kupokea ipasavyo kile ambacho Bwana anasema nawe.

Utakuta mtu anakuja ibadani saa nne mpaka saa tano asubuhi hali ibada inaanza saa tatu asubuhi;na hali akijua muda wa kuanza ibada. Lakini haumii hata kidogo wakati akichelewa ibada,utakuta mtu huyo akiona ni sawa tu!. Lakini mtu huyo huyo ukimuona jinsi anavyowahi asubuhi kwenda kazini utashangaa! tena utamkuta akiwa tayari hata kushuka katika dala dala wakati wa foreni na kuchukua boda boda kusudi tu awahi kazini ,asifukuzwe kazi. Lakini Mungu je ampaye nguvu za kufanya hiyo kazi kamuacha !!!

Haya ndio mazoea na yanakuwa adui katika mafanikio yako. Emu jaribu sasa kuenenda kinyume na desturi na mazoea;ikiwa kama utachelewa aua kukosa ibada moja basi usikie kuugua/uumie ndani ya moyo wako. Ukitaka kufanikiwa kiroho na kiuchumi basi dawa ni kukataa desturi/mapokeo yasiyo na maana pia kataa mazoea katika suala linaloitwa ibada.

Kwa msaada wa maombi piga;+255 683 877 900

What’s app number ni+255 746 446 446

ITAENDELEA…

Mchungaji G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page