top of page

UPENDO / LOVE.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Upendo ni amri iliyo kuu tena ndiyo amri ya kwanza ( Mathayo 22:37-40). Na katika upendo amri zote na unabii wote unashikiliwa hapo ( All the Law and the Prophets hang on these two commandments.”).Hivyo, Upendo ndio utimilifu wa sheria ( Warumi 13:10). Hii ina maana kule kusema usiibe,au usizini ; amri zote hizo hutimilika katika pendo,kwa maana katika pendo huwezi kuiba,wala kuzini. Tena hii ni sawa na kusema yeyote anayependa ameshika amri zote. Kipindi cha agano la kale kilikuwa ni kipindi cha sheria,lakini sasa ni kipindi cha kuwa na uhusiano / ushirika ( Fellowship) na Bwana, katika pendo pekee ndipo ukamilifu wa ushirika ulipo.

Kuna aina kuu mbili za pendo;

  1. Upendo wa Mungu ( God’s love)

  2. Upendo wa binadamu ( Human love)

01. Upendo wa Mungu.

Mungu mwenyewe ni “pendo ” ( 1 Yoh.4:8,16). Si tu anatupenda bali Yeye ndiye pendo lenyewe. Hata hivyo Mungu anatupenda sio kwa sababu tunastahili kupendwa naye,bali ameamua kutupenda kwa pendo lake. Pendo lake ni la milele ( Yer. 31:3),hii ina maana vile anavyokupenda jana ndivyo akupendavyo leo,upendo wake haujawahi kubadilika,na kamwe hauwezi kubadilika,wala kubadilishwa na kitu chochote. Katika pendo la Mungu,mambo matatu muhimu kujua;

a)Aliupenda ulimwengu ( Yoh.3:16)

Huu ni ulimwengu wenye dhambi,uovu wa kila aina ndio alioupenda Mungu. Ni sawa kabisa kusema hata mwenye dhambi wa leo,bado Mungu anampenda. Hata jambazi wa sasa ambaye bado hajatubu wala yule asiyekuwa na mpango na Mungu,lakini bado Mungu anampenda bado,kwa sababu ni mtu wake. Mfano mzuri,ni pale tunapoliona pendo la Mungu kwa Zakayo mtoza ushuru,lakini bado Yesu alimfikiria na kumwambia “ leo wokovu umefika nyumbani humu,kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu“Luka 19:9

b) Pendo la Mungu kwa Yesu, Mwana pekee. ( Mathayo 3:17,Yoh.17:5)

Ni vyema kufahamu kuwa Yesu na Baba,(Mungu) ni umoja ( Yoh. 10:30). Katika hili,Mungu amedhihilisha pendo lake kwa Yesu Kristo kwa maana wao ni umoja pamoja na Roho mtakatifu.

c) Kwa sababu anatupenda,anaturudi ( Waebrania 12:6-11)

“ Marudia” hueleza namna gani Mungu anavyotupenda kwa maana kwa sababu ya pendo,Bwana huturudi/ Yeye hutufundisha nidhamu ya maisha. Kama vile unavyoweza kumfundisha nidhamu mwanao si kwa lengo la kumuumiza bali kwa sababu hutaki apotee,hivyo unamfundisha nidhamu. Pendo la Mungu linasababisha marudia kwetu,ili tusije kupotea. Wakati mwingine Mungu anaweza akaruhusu tupite kwenye moto,kama sehemu ya kutunuoa imani yetu,au pale tunapokuwa na shingo ngumu anaweza kuruhusu magumu fulani yatupate ili kusudi tujifunze. Hayo yote ni sehemu tu ya marudia yanayoonesha pendo la ajabu kwetu.

d) Wokovu ni pendo la Mungu. ( Yoh.3:16)

Pendo la Mungu linaonekana wazi kupitia kazi ya msalaba. Ukweli ni kwamba kazi ya msalaba ni kamilisho la pendo la Mungu kwa watu wote,ili kwamba “tuokoke” tusipotee. Mungu amefunua pendo lake kwetu sisi kupitia Kristo kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi ( Warumi 5:8). Hivyo,tunapouangalia msalaba wa Yesu,tunaliangalia pendo la Mungu kwetu sisi watu ambao tulistahili hukumu ya moto! Kwa pendo lake amemtoa Yesu,awe fidia ya wengi ( Mathayo 20:28),na kupitia Kristo wewe uokoke/ uokolewe. Huu ni upendo wa namna gani wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya mtu mwingine? Hakika ni upendo wa ajabu usioweza kuelezeka.

  1. Kusudi la pendo la Mungu.

~ Watu warejee kwake / waokoke kwa kumwamini Kristo na kumpokea ( 2 Petro 3:9,1 Timotheo 2:3-4)

02.Upendo wa binadamu ( Human love)

“Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,Kwa kuwa amenijua Jina langu.” Zab.91:14

Andiko hilo hapo juu,linaeleza kuwa mtu anaweza kumpenda Mungu, ndio maana aweza kuokolewa. Hata hivyo Mungu haokoi kwa sababu tunampenda,bali kwa sababu amepanga atuokoe. Katika pendo la mwanadamu,na lenyewe limegawanyika sehemu mbili kuu,kama ifuatavyo;

a) Upendo wa mtu kwa Mungu ( Marko 12:30) ~ Kwa kuwa hatupo tena chini ya sheria,bali katika neema. Hivyo,kumpenda Mungu hakuji kwa sheria bali katika uhusiano wetu mzuri mara baada ya kumpokea Yesu/kuokoka. Tukimpenda Mungu, taratibu zake Mungu zi nzito ( 1 Yoh.5:3). Upendo huu ndio upendo wenye kutusumbua sana, kwa maana si wengi wanaompenda Mungu. Na shida ya upendo kwa ujumla wake hupatikana kwenye eneo hili!!!

b) Upendo wa mtu kwa mtu ( Yoh.13:34) ~ Upendo wa namna hii unaweza ukawa ni upendo wa mwana ndoa kwa mwanandoa – Mithali 5:18-19 ,jirani kwa jirani,adui kwa adui ( hata majambazi hupendana),mtu na mtoto – Mwanzo 22:2.

  1. Kwa nini leo hakuna Pendo halisi?

Leo kuna shida ya watu kupendana ingawa tunaweza kupendana. Mbaya zaidi wasiomjua Mungu wanaweza kupendana katika dhambi,na uovu wao lakini wapendwa wakachukiana tena kanisani!!! Ukiona watu hawapendani,basi ni dhahili watu hao hawana mahusiano mazuri na Mungu. Au kwa maneno mengine,“hawampendi Mungu ” la kama watasema wanampenda basi si kweli,ni waongo kwa maana neno la Mungu linasema “ Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” 1 Yoh. 4:8. Kwa hiyo,leo; tumekuwa mbali na pendo halisi kwa sababu hatumpendi Mungu ingawa na kanisani tunaenda. Kwa maana wanaompenda Mungu ndani ya kanisa ni wachache sana tofauti na unavyofikiria,wengi wanaigiza tu.! Mungu atusaidie.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp +255 746 446 446

Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page