top of page

ACHILIA NA UVUKE!

Updated: Aug 26, 2022


Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.” Mwanzo 33:4 (KJV)


Bwana Yesu asifiwe…


Kwa ufupi,


Biblia inatueleza kuhusu mapacha wawili Esau kaka mkubwa na pacha wake Yakobo . “kulwa na doto” wa baba na mama mmoja ( Isaka na Rebeka). Watoto hawa mapacha walifarakana tangu wakiwa tumboni ( Mwanzo 25:23). Hivyo tofauti zao sio za kawaida, zilikuwa ni tofauti za ndani hasa. Biblia inasema “mkubwa( Esau) atamtumikia mdogo”.

Baada ya miaka mingi ya uhasama kati yao,na baba yao Isaka alipokufa. Esau alikusudia kumwua ndugu yake ( Mwanzo 27:41).


Hivyo ndani ya Esau kukawa na mipango ya kumwua mdogo wake kwa sababu ya mbaraka ambao Yakobo alibarikiwa na baba yake.

Shina la uchungu likachipuka kwa Esau,roho ya mauti ikamsimbua,harufu ya damu ikasikika moyoni mwake. Kwa neema ya Bwana Yakobo akambia muuaji. Lakini Esau akaendelea kumshikiria ndugu yake moyoni kwa muda mrefu akitafuta amwangamize.


Hivi ndivyo hata leo,watu wanatembea huku wakiwa wamewabeba watu mioyoni mwao. Kwa sababu tu ya makosa ya kale. Leo kuna akina Esau ambao wanasumbuliwa na shina la uchungu. Angalia hapo, Esau aliangaika sana na maumivu ya moyoni kwa sababu tu ya mbaraka!!!


Kwa sababu hiyo, Esau alikuwa nje ya milango ya baraka iliyokusudiwa. Tena akawa kinyume na matakwa ya wazazi kwa maana alienda kuoa mahali ambapo hayakuwa mapenzi ya wazazi wake. Kwa sababu Esau aliendelea kuishi huku akiwa amesmshikilia ndugu yake,hali hiyo ikampelekea yeye na kizazi chake kuwa na chuki mbaya dhidi ya kizazi cha Yakobo/ Israeli,chuki ikazaa kiburi ( Obadia 1:3)


Kawaida ya kumshikilia mtu aliyekukosa inapelekea kuambukiza ukoo au familia yako na hatimaye utakuta familia nzima inachukia familia ya pili hata kama watoto walikuwa hawajui asili ya chuki hiyo. Leo tunao watu ambao wamebeba chuki dhidi ya mtu,na hatimaye akajikuta ameambukiza watoto wake kumchukia huyo mtu. Kama ilivyokuwa kwa Esau na kizazi chake dhidi ya Yakobo na kizazi chake.

Esau ageuka na kumwachilia Yakobo

  1. Mungu mwenyewe aliamua kumgeuza Esau na kuhakikisha uchungu wake unafikia mwisho. Lakini biblia inatuambia hali hii haikuja automatically Bali Yakobo aliomba ( Mwanzo 32:11). Hii ni sawa na kusema “maombi ya Yakobo “ yalimaliza uhasama wa kaka yake.

Nguvu ya mungu ilipenya moja kwa moja na kupasua moyo wa chuki, uhasama na mauti iliyopo ndani ya Esau na hatimaye Esau kwa kuthibitiwa na nguvu ya Mungu kama alivyoomba Yakobo, Esau akatulizwa. Kumbe! Ukiwa na ndugu aliyebeba chuki Kali kiasi cha kutamani kifo,ukiomba,aweza kugeuzwa na kuwa mtu mwingine. Maana Esau aligeuzwa. 

Esau akaachilia chuki,na kujikuta akimkumbatia ndugu yake Yakobo na hapo hapo alipoachilia hayo,tunaona upendo wa mapacha ukionekana kwa kuanza kuoengea Kila mmoja kwa upole sana. 


Kumbuka;


ukimshikilia mtu kwa sababu ya makosa yake ya zamani,ni wewe ndio utakayejifungia milango Yako ya baraka. Bali ulimwachilia utavuka.

Biblia haituambii kwamba Yakobo alimtafuta nduguye kwa kuomba msamaha. Bali Yakobo aliomba kwa Mungu,Kisha Mungu alisikia na kumtengeneza Esau.


Kuna wakati kwenye maisha huwezi kusubiri mpaka aliyekukosa aje kisha aombe msamaha ndipo umwachilie,bali waweza kumwachilia na makosa yake hata kabla ya kuomba msamaha kama vile Esau alivyomwachilia Yakobo kabla hata ya kukaa chini na kuongea. 


Ikiwa umebarikiwa, nifahamishe kwa+255 683 877 900


What’s app + 255 746 446 446.


Na Mch. Gasper Madumla


UBARIKIWE

Recent Posts

See All

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page