top of page

UNATAKA KUWA MZIMA?

Updated: Sep 29, 2022



“Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yoh.5:6


Siku moja Yesu alikwenda Yerusalemu, na huko karibu na mlango wa kondoo ( sheep gate),kulikuwa na kisima chenyemaji yaponyayo pale malaika akishuka na kuyatibua. Uponyaji wa maji haya ulitegemea “kushuka kwa malaika” na kuyatibua maji. Na hapo katika wagonjwa hao,kulikuwa na mmoja ambaye alikuwa mgonjwa muda mrefu wa miaka thelathini na minane. Kumbuka,biblia imetaja muda wa miaka aliyokuwa akiumwa kwa makusudi kwamba tuelewe alikuwa kweli ni mgonjwa mwenye mateso makali. Wakati wakisubilia maji yachemke,na malaika ashuke,hapo ndipo Yesu naye akashukia kwenye kisima hiko hiko ( wasijue Yeye Yesu ndiye zaidi ya malaika aponyaye).


Wale wagonjwa wameketi wakisubiri,lakini hawaoni huyo malaika isipokuwa wanamuona Yesu,nao wamekaa wengine wamelala wakisubiri huyo malaika. Tunajifunza kitu hapo,kwamba wakati mwingine Yesu ameshuka tayari kukuponya labda kupitia mtumishi wake yeyote yule ambaye wala sio mchungaji, lakini wewe unakaa ukimsubiri mchungaji mwenyewe aje ndio upokee. Mungu huwatumia watu mbali mbali,lakini shida kubwa ni mtazamo mbaya uliopo ndio unakwamisha imani,na uponyaji wenyewe.Yesu alipomwendea yule mgonjwa alimwuuliza swali moja tu “ wataka kuwa mzima?” mimi nalitazama swali hili kwa jicho la utofauti kidogo,kwa maana najiuliza kwanza;


  1. Kwa nini Yesu anamwuliza mgonjwa swali hili? Hali akijua mgonjwa anahitaji uzima.

  2. Kwa nini asimponye tu,kisha amwache aondoke zake

  3. Kuna uhusiano gani katika swali hili na maisha yako ya sasa?

  4. Nini hasa chanzo kikubwa cha magonjwa?

  5. Vipi wagonjwa wenzake,walijisikiaje wakati Yesu anamwuliza mgonjwa mmoja tu habari ya uponyaji wake

  6. Wayahudi nao wamemchukuliaje Yesu? Wamemchukuliaje yule mgonjwa?


Bila shaka kuna maswali mengi mno ya kujiuliza,ninayo mengi. Lakini kwa hayo machache tunaweza kuona kitu kikubwa sana,nami nikagundua baadhi ya majibu yake machache. Katika ujumla wake,kwanza kabisa; Yesu Yeye ndiye mponyaji mkuu,ameshuka pale kisimani lakini wagonjwa wameshindwa kumwendea kwa maana labda hawakumtambua kwamba Yeye ndiye hasa huyo malaika aponyaye,na sasa ameshuka kwa ajili yao. Na ndivyo ilivyo hata sasa,wengi hawaamini sana bali wana mashaka katika uponyaji alionao Yesu.


01. Kwa nini Yesu alimwuliza swali hilo? – Bila shaka Yesu alimtaka mgonjwa “aombe “. Yesu alifahamu ugonjwa wote pamoja na mateso yote aliyokuwa anapitia mgonjwa, hii inatuonesha kwamba hata sasa ndiye ajuaye ugonjwa wako,mateso yako yote,na vyote unavyopitia. Lakini Yeye bado ametoa nafasi kwako usimame na kuomba ili upokee uponyaji. Swali hili,Yesu anakuuliza na wewe “Wataka kuwa mzima?” yaani hali akijua ugonjwa wako lakini anataka utamke,useme / umwombe Yesu aponyaye Yeye ni Yehova Rafa ( Bwana aponyaye).


02.Kwa nini asingemponya tu,basi yatosha. – Mungu ametupa nafasi yetu ya kufanya naye ana nafasi yake ya kufanya. Ukweli ni kwamba siku zote yeye huponya kwa utukufu wake mwenyewe sio kwa kulazimishwa. Naye wakati mwingine huponya hata bila kuopwa,lakini mara nyingi ametupa nafasi tuombe. Kupitia mgonjwa huyo,Yesu anatufundisha somo la maombi


03. Uhusiano wake ukoje wa swali hili na maisha yako?


Ni ukweli hata leo tunaumwa bado. Wewe pia labda nawe unaumwa hata sasa,lakini unaombaje pale unapoumwa? na huo ndio uhusiano tunaouona. Ebu angalia aina ya maombi aliyokuwa akiomba yule mgonjwa wa miaka 84,pale Yesu alipomwuuliza “wataka kuwa mzima?”,yeye alijibu katika namna ya ”malalamiko” akiwalaumu wengine wanaomtangulia mbele yake (Yoh.5:7).


Ni kweli kabisa alivyojibu,lakini Je ndio aina nzuri ya maombi mbele za Yesu? Ukichunguza kwa undani utagundua kwamba maombi yake ya kutaka kuponywa yalikuwa yakizunguka sana,hakuwa na hoja yenye nguvu,naye alijaa kunungunika mno ! Lakini ndio aina ya maombi tunayoyafanya mbele za Bwana leo!!! Tunahitaji kuponwa lakini maneno yetu hayaeleweki kama kweli tunahitaji kuponywa. Ni vyema ukajifunza kuwa na maombi ya moja kwa moja kueleza hasa unataka Bwana akutendee nini? Bila kulalamika katika maombi yako.


04. Nini hasa chanzo kikubwa cha magonjwa? 


Bila shaka vyanzo vya magonjwa vipo vingi mno. Kwa maana katika hali tu ya kawaida,magonjwa mengi husababishwa na vyakula tunavyokula,vinywaji tunavyotumia,hali ya hewa tunayovuta,kutozingatia kujali afya zetu n.k. Lakini chanzo kikubwa sana ni “dhambi”,karibuni asilimia 80 hivi ya mateso tunayopitia leo hutokana na dhambi. Kwa mujibu tu,wa kisa hiki (Yoh.5:14) Tunaona ni kwa namna gani dhambi ilivyomlaza mtu muda wa miaka 84,ilikuwa imwondoe uhai kabisa!!! Hivyo,utagundua jibu la swali hilo unapoulizwa “unataka kuwa mzima?” ukisema “ndio nataka” basi hoja itakayofuata ni “angalia umekuwa mzima,usitende dhambi tena,usije ukaanguka kwenye ugonjwa mbaya zaidi ya huo”. Lakini tunafahamu kwamba si wote wanaumwa wametenda dhambi ,isipokuwa wengi ni kwa sababu ya dhambi!!!

5 & 6 Nini matokeo ya kuponywa? – Wayahudi hawakufurahi kabisa kwa maana Yesu alitenda hayo siku ya sabato na hawakujua Yeye mwenyewe ndio Bwana wa sabato. Hali hii ipo hata wakati huu hapo kwako,kwa maana unapoponywa na Bwana,wapo watu ambao hawatafurahia. Watu hao mara nyingi wanatamani kukuona mgonjwa siku zote. Lakini wamesahau kwamba wewe ni mali ya Bwana na kuna siku utakuwa mzima,lakini upo tayari kuponywa?


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI,piga sasa kwa namba hizi;

+ 255 683 877 900


Whatsapp namba +255 746 446 446


Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

Opmerkingen


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page