KUSHUGHULIKIA LAANA YA UKOO
- Mch. Gasper Madumla
- Mar 13, 2017
- 2 min read

Na Mch.G.Madumla
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Kusema ukweli pamoja na kwamba weweza ukawa umeokoka vizuri kabisa lakini mambo ya laana katika ukoo/familia yako ikawa inasumbua mpaka sasa. Unajua nyingi za kikwetu Afrika zilikuwa ni za kuabudu miungu ya jadi,matambiko na makafara. Hivyo si rahisi mambo yote hayo kuondoka mkwa mara moja tu! Ukweli ni kwamba ukiokoka,laana haina nguvu kwako,
kwa maana Yesu Kristo alikwisha shughulikia laana zote pale msalabani kwa ajili yako.Lakini shida inakuja kwa upande wa ukoo au familia yako ambayo bado inatembea kwenye laana. Unajua kuna familia ambazo zimeandamwa na majanga kila mwaka,yaani janga juu ya janga tena kwa bahati mbaya hata kuelewana hawaelewani,
tena ndugu hawafahamiani kabisa (Wenye kufahamiana ni ndugu wachache,bali wengi hawajuani wala kufahaminiana). Tena zaidi ya hapo familia nyingine zimepigika hatariii! kiasi kwamba hata nyumbani (kule kijijini) ardhi ni kavu yaani hailimiki.
Hali ya namna hii sio hali ya kawaida,ukiona kwenye familia yako basi ujue kuna shida ya kiroho iliyofanywa na mababa watangulizi/viongozi waliotangulia. Na ndio maana hata wakati wa Daudi kulikuwa na njaa muda wa miaka mitatu mfululizo,Daudi akaamua kuutafuta uso wa Bwana naye Bwana akamjibu kwamba ni kwa sababu ya Sauli mtangulizi wake aliyekorofisha kiasi kwamba nchi akakubwa na shida Soma (2 Samweli 21:1-2)
Kumbe mtangulizi wako ikiwa kama kaharibu kiroho kuna uwezekano wengine kuendelea kupitia katika majanga. Sasa jiulize tu,ni mara ngapi wazee wetu wa kiukoo wamekorofisha kiroho? Ni mara ngapi waliua na kisha damu wakamwaga malangoni huko katika miji tulikotoka bila sisi leo kuwa na ufahamu wowote tena kwa bahati mbaya nao/wazee hawapo sasa walikwisha kufa muda mrefu sana!(Kama alivyofanya mzee Sauli kisha akajifia na kuacha laana kwenye ardhi,cha moto wakakipata wengine)
Mambo ya kushughulikia.
01.Ikiwa wazee kama bado wapo hai,wadodose wakujuze zaidi.
Unajua kama umepata neema ya kuwa na wazee mpaka sasa,basi hakuna sababu ya kudhani au kufiria fikiria bali anza kuwadodosa dodosa kwa lengo la kutafuta mahali pa kuanzia kupashughulikia. Pamoja na uwepo wa Roho mtakatifu atakayekusaidia katika kila hatua but,
kama wazee wapo hai,usiwaache hao bila kuwasumbua sumbua kwa maswali kadha wa kadha,maana hujui wewe kwa nini Mungu amewaacha hai mpaka umri huo,labda Mungu amewaacha kwa kusudi hilo hilo la kushughulikia yaliyofanywa hapo zamani kipindi wao wakiwa vijana,ila wameona baba zao wakifanya vitu vya ajabu! hao ni mtaji wa kuanzia.
02. Maombi yafuate;
Omba toba (Kwako mwenyewe,kwa ardhi,kwa walioshiriki ama kushirikishwa,kwa wazee wenyewe,pia toba kwa ukoo na familia nzima)
Omba msaada wa Roho mtakatifu ( Akupe maelezo ya namna ya kualianzia jambo hilo,Yeye atakuongoza nini unapaswa kufanya na nini hupaswi kufanya,omba mafunuo ili ujue siri za familia n.k)
Toa nafasi ya watumishi wa Mungu wakusaidie
Neno linaendelea kuchapwa. (HIVI PUNDE LITAKUWA TAYARI,USIONDOKE!)
Kwa maombezi,nipigie sasa kwa +255 683 877 900
What’s app ni +255 746 446 446
Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
コメント