top of page

UJUMBE WA SIKUKUU


Mch.Madumla

Na Mchungaji Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Ni ukweli usiopingika kwa kila mtu aaminiye na hata yule asiyeamini kwamba hivyo ulivyo sasa ni Mungu pekee amehusika asilimia zote. Tazama ni wangapi uliokuwa nao lakini leo hawapo wamekufa,au ni wangapi waliotamani leo wangelikuwa kama wewe kwamba wawe na afya kama yako,wawe na viungo vya mwili kama vyako,lakini wengine wamelazwa hivi sasa,wengine wamevipoteza viungo vyao vingine kwenye ajali au magonjwa, JE WEWE NI BORA KULIKO WAO?

Ni lazima tukubaliane hapa kwamba ni kwa rehema na neema tu hata leo umefika hapa. Hivyo basi,katika mambo hayo yote yatupasa kushukuru MUNGU sana. Unajua hata huwezi kuamini amini ya kwamba mwaka ndio umeisha hali wewe u mzima. Nami nilipoliangalia jua leo asubuhi nikasema hakika ni Ebeneza,tazama imekuwa ni siku mpya kwa utukufu wa Bwana maana kumbuka kila siku ni siku tukufu kwa Bwana.

Sikukuu ya mwaka mpya ni siku ya kumshukuru Bwana Mungu kwa yote aliyokutendea. Siku hii siyo siku ya kufanya zinaa kama wengine wanavyoitafsiri,bali ni siku ya kuikimbia zinaa (1 Wakorintho 6:18).Siku hii yakupasa pia,ukae na familia yako ukitafakari matendo makuu katika familia yako. Ni siku ya kucheka na mkeo/mumeo/watoto na ndugu zako.

Watu walio ovyo,wanaitumia siku hii kwa kufanya maovu sawa sawa na matakwa yao yasiyompendeza Mungu,bali mimi nakushauri uchague kutenda mema siku hii na siku zako zote maana kumbuka hujui siku wala saa utakapokufa,saa ya kujitayarisha ni sasa,yaani saa iliyokubalika na wakati wa wokovu ni sasa~2 Wakorintho 6:2.

Wewe baba,utulie na familia yako,haipendezi sikukuu yote hii ukawa unazulula zula peke yako. Basi kama kutoka toka na familia yako. Na wewe mama,jitulize na familia yako leo. Tena mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu na kumshukuru Mungu Baba katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo. Waefeso 5:20

Ni muhimu kuingia mwaka kwa maombi ya ushindi,hivyo yakupasa uombe. Na ikiwa utahitaji maombezi tafadhali unipigie kwa simu hii;+255 683 877 900.

▪Nami nakutakia sikukuu njema mpendwa, uzidi kubarikiwa.

What’s app +255 746 446 446

MchungajiGasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page