top of page

SIFA NA KUABUDU ~03

Updated: Sep 29, 2022


  • Wimbo wa ushindi ( wimbo wa Musa na Miriamu) – Kutoka 15:1b – 18

“Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema,….15:1a,.” Musa,Haruni na Miriamu kama viongozi wa kusanyiko ,watu hawa nao waliimba pamoja kusanyiko lote. Hii inatupa habari kwamba kama kiongozi wa kusanyiko / kanisa huna budi kuimba na kuabudu pamoja na kusanyiko, kumbe! Kazi ya sifa na kuabudu ikiwa inafanyika katika kusanyiko / kanisa inamtaka na mchungaji kiongozi,pamoja na wachungaji,wazee wa kanisa, viongozi wengine pamoja na kusanyiko lote,


wasifu na kuabudu pamoja. Si jukumu la waimbaji peke yao,bali waimbaji wasimame kama viongozi wa ibada ya sifa na kuabudu, lakini “kusanyiko lote na limwimbie Bwana “. Musa kama kiongozi mkuu wa msafara,naye alihusika kwenye sifa na kuabudu. Lakini leo naziona changamoto kubwa,kwa maana viongozi wengine wa kanisa, hawashiriki ibada ya sifa na kuabudu, isipokuwa wanakaaga ofisini wakisubiria muda wao wa kuhubiri / kufundisha ufike ndipo waelekee madhabahuni.


Na viongozi wa namna hii,siku zote wanatabia inayofanana ya kuondoka ibadani pale wanapomaliza kuhudumu,kwa hiyo kama kuna sifa itafuatia au watu wataabudu,hiyo wao ni kana kwamba haiwahusu!

Lakini sivyo maandiko yasemavyo,sijui utaratibu huu wameupata wapi.!!! Biblia inatuambia Musa kamanda in charge,Miriamu na kusanyiko lote,wakaimba pamoja,ndivyo biblia isemavyo.


Kama waimbaji wa siku za leo,lazima kujifunza kwa kina juu ya “wimbo wa ushindi” ambao unajenga msingi wa utunzi na uimbaji mbele za Bwana. Ibada ya sifa na kuabudu si ibada ya kawaida kawaida,bali ni ibada yenye nguvu,ambapo mwimbaji lazima ajue ni nini hasa anaimba! Wimbo Musa na Miriamu pamoja na Israeli hujulikana pia kama wimbo wa ushindi kwa sababu Bwana aliwashindia Israeli dhidi ya watesi wao Wamisri waliowatumisha kwa miaka 430.


Israeli alipotolewa utumwani,hapo walikusanyika na kumwimbia Bwana. Kiini cha wimbo ni kumsifu na kumwabudu Mungu,wimbo haukumsifia Musa,wala Haruni wala Miriamu bali Mungu tu. Na ndivyo kiini cha “sifa na kuabudu ” kinavyopaswa kuwa,sifa zote ni za BWANA Mungu tu( Ukiona sifa zinaelekezwa kwa mwanadamu,ujue hiyo sio ibada ya sifa inayostahili kuwa!).

Wimbo wa Musa na Miriamu, umegawanywa katika beti/maeneo mawili muhimu.( Ingawa yanaweza yakawa maeneo matatu)

  1. Fungu la mstari 2-6,7-11 ( sifa juu ya ukombozi.)

  2. Fungu la mstari 12-17 ( Sifa juu ya unabii wa kuingia Kanaani,nchi ya ahadi)

Mafungu yote mawili,yanatoa picha kwa habari ya sifa na kuabudu kunakoweza kufanyika leo, iwe ni kanisani au popote pale. Kwa mfano;


01. Fungu la kwanza ( Ukombozi)


Ibada ya sifa,inapaswa ielekeze jicho lake juu ya “ukombozi” kwa kumwinua Kristo Yesu,Yeye aliyekomboa maisha yetu. Katika kundi hili,Kiini haswa ni ukombozi,Yesu asifiwe na Mungu baba vivyo hivyo. Kumbuka kiini hiki,Bwana pekee ndiye wa Kusifiwa kwa maana kwa mkono wake hodari Israeli alikombolewa,na ndipo hata sasa focus/ kiini kinabakia pale pale. Wimbo,unaanza na kiitikio chenye nguvu,“ Nitamwimbia Bwana,kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini” ( 15:1b,2b).


Lakini si tu hapo,katika fungu hili la kwanza,mwimbaji anapata changamko la moyoni kiasi cha kutaka kumfahamu zaidi Bwana, hata akamweleza Bwana katika taswira ya “mtu” 15:1a,lengo hasa nikueleza ni kwa namna gani Bwana anavyowapigania watu wake.n.k Kwa hiyo, kila mstari unaeleza matendo makuu ya ajabu aliyoyafanya Bwana kwa uweza wake. Hili ndilo kundi la sifa!


Hata hivyo mtunzi wa siku za leo, hana budi kupitia mistari yote ya sifa,na kutafakari kuona ni kwa namna gani naye atamsifu Mungu tu. Kwa maana kama hataweza kufanya hivyo,anaweza akajikuta anapata hasara kwa kuacha kumsifu na kumwinua Bwana atoaye “ukombozi” na badala yake akajikuta akijisifia yeye mwenyewe,au kumsifia mtu,au akajikuta akieleza shida na matatizo yake binafsi na kisha akauita wimbo wake ni wimbo wa sifa!!! Kumbuka; Fungu la kwanza la wimbo huu,linajaribu tu kutoa picha ya ujumla juu ya sifa iweje siku za leo.


02. Fungu la pili ( Unabii juu ya nchi ya ahadi)


Kwa kuwa Israeli alikuwa bado yupo safarini kuelekea nchi ya ahadi. Kwa maana kutoka utumwani hakuna maana ya kwamba wamekwishika nchi ya ahadi,wali walikuwa njiani kuelekea Kanaani yao. Hivyo,picha kubwa ilikuwa katika kumtegemea Bwana atakayewafikisha nchi ahadi. Kitendo cha kumtegemea Bwana, kinaonesha tendo la “ kuabudu” . Tendo la kuabudu linaeleza kuziona ahadi zijazo kana kwamba wamekwisha zipokea. Katika sifa na kuabudu kunajengwa na “tumaini jipya la wokovu katika Kristo, Yeye anayestahili kuaminiwa”…


ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI,


piga kwa +255 683 877 900


Whatsapp namba .+255 746 446 446


Mch.G.Madumla 2014


UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page