NJIA YA UZIMANI,IMESONGA!
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 1, 2015
- 2 min read
Updated: Sep 5, 2022

Njia ya uzimani,imesonga ( difficult to travel is the path that leads the way to [everlasting] life, and there are few who find it.)
” Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. ” Mathayo 7:13-14
Kwa kawaida njia ya upotovu ni pana,kwa maana wengi hukimbilia huko. Kwa maana njia pana ni rahisi kupita /kusafiria (Na ukumbuke ya kwamba watu hupenda njia fupi). Lakini ni tofauti na njia nyembamba ambapo kwanza kuiona ni kazi! lakini ni wachache wenye kuweza kuiona njia hiyo. Katika mfano huu ambao Yesu alikuwa akifundisha,alikuwa anatoa picha halisi juu ya safari ya kwenda uzimani kueleza kwamba safari si rahisi tena haiwezekani bila Yeye.
Katika kipindi cha Yesu kulikuwa na njia pana ambapo wasafiri walizitumia kusafirishia ngamia zao na misafara kadha wa kadha,katika njia hizo – watu walizipenda kwa maana zilikuwa zina nafasi ya kutosha. Lakini cha ajabu ndio zilikuwa ni njia ambazo wengi waliangukia pabaya,kwa maana wengine walijikuta wakiangukia kwa wanyanganyi (Luka 10:30). Lakini hata hivyo kulikuwa na njia nyembamba / vichochoro ambayo si wengi walikuwa wakivitumia,kwa maana vimesonga mno,lakini pia cha ajabu njia hizo zilikuwa hazina uharibifu kama ule wa njia pana.
Kwa ufahamu huo,njia ya uzima inatoa picha kwa msafiri katika maeneo yafuatayo
Kuitafuta.
Kwa kuwa ni njia nyembamba na mlango ni mwembamba,msafiri hana budi kuutafuta. Kwa maana hauonekani kwa kila mmoja,lakini akiutafuta,hakika unapatikana. Yesu Yeye mwenyewe ndiye Njia (Yoh.14:6). Mtu anayemtaka Yesu lazima amtafute,kwa maana si wengi wenye kumwona. Lakini yupo hai na anapatikana kwa wotewatakaomtafuta (Isaya 55:6).
Kukubali kuacha mizigo,ili upite njia / mlango mwembamba.
Kawaida ukitaka kupita katika mlango na njia nyembamba itakulazimu ukubali kuacha mizigo ili upite wewe kama wewe. La kama utakwenda na mizigo yako basi uwe na uhakika utakwama hapo katika mlango mwembamba. Kwa maana njia / mlango ni mwembamba mno. Leo katika safari ya wokovu,ni lazima ukubali kuyaacha mambo mengine ili ufanikiwe kuuona mlango wa uzimani ( Kumbuka ; Dhambi ni mzigo mkubwa sana,
na usidharau ili,shughulikia sasa). Lah! kama unakubali kwenda nayo mambo yote,basi ni ukweli kwamba,hutaweza kutembea vyema katika wokovu wako sasa,na mamizigo yako yanaweza kukukwamisha kuuona uzima wa milele. Soma habari za Yona;
pale walipoona kwamba wanaelekea kuzama,iliwalazimu kushusha mizigo/shehena baharini ili wasipotee na wao,wakafanya hivyo kuinusuru merikebu yao na safari nzima,lakini hata hivyo waligundua mzigo mkubwa haukuwa gunia za mchele bali alikuwa ni mwanadamu Yona aliyejichimbia chini,akalala,huyo ndiye alikuwa ni mzigo wa kukwamisha merikebu kwa vile alivyomkimbia Bwana. Hata Leo mwanadamu amekuwa ni mzigo mkubwa sana,ukimwendekeza mwanadamu basi ujue hapo huwezi kusonga mbele katika safari yako ya wokovu.
Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,
Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900
What’s app namba ni+255 746 446 446
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários