MWAKA WA MAFANIKIO.
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 31, 2017
- 3 min read

Anaitwa Deogratius, a.k.a Deo mnyamwezi,Deo mnyama,kijana fulani hivi,mjanja mjanja kutoka pande za Sinza ( Data es salaam Tanzania,Tz) kwa wajanja.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
huyu jamaa ana ndoto za ajabu ajabu, mara oh anataka kuwa lubani wa ndege,mara oh anataka kuwa baharia,mara oh anataka afisa TRA yaani mipango mingi na shule hakuna!!! Lakini mipango yote hiyo ni kwa sababu jamaa anataka “kutoka” kimaisha,
Ninachompendea huyu jamaa wa kufikirika ana mishe-mishe nyingi,mtu wa madili kila kona lakini wapi life bado hajalipatia. Kumbe kufanikiwa katika maisha sio jambo la mara moja ,kuna mchakato wake! Uzuri mwingine wa mshkaji huyu hakati tamaa,anapambana kiume!!! Na wakati mwingine anapata hasira anapoona “watoto wa mama” wanaendesha mandinga ( magari) ya baba zao kilaini tu,wakati kidume anasota mtaani.
“ Ila poa,ipo siku tu” ndio maneno ya jamaa akiamini kuna siku atatoka kimaisha. Ndoto zake ni kwenda mamtoni/ ulaya. Ila ndio mipango bado! Ila tatizo naye anajichanganya sana na wahuni,Kwa hiyo anachokipata kinaishia kwenye pombe na ganja.
Tunamsaidiaje Deo ili atoke mwaka huu?
Hilo ni swali ambalo najiuliza Mimi kwa kijana kama Deo,maana wapo wengi wenye usongo wa kutoka ila michakato hajakaa sawa. Najaribu tu kufikiria baadhi ya njia sahihi za kufanikiwa katika mwaka huu,nayo ni;
01.Kaza katika ibada
Kijana kama Deo,laiti kama atalitambua umuhimu wa kutengeneza maisha yake kiibada hakika atakuwa na mtazamo sahihi. Kwa sababu kuna starehe ambazo hataweza Tena kuendelea nazo. Na kwa sababu hiyo,ataweza kutunza kile kidogo akipatacho kwa matumizi mengine yenye umuhimu. Fikiria kaingiza Tshs 10,000 Kwa siku na kufanikiwa kutumia 5,000 kisha kuweka 5000. Ujue huo ni mwanzo mzuri wa kufanikiwa kwake.
Hata wewe ni lazima kama unataka kutoka ujikite tiki tiki kwa Bwana,kwa maana yeye ndiye chanzo na sababu ya kufanikiwa kwako. Hivyo ni lazima ujitahidi sana katika mwaka huu kumshika Bwana. Ikiwa kama miaka iliyopita ulikuwa mbali kiibada,Basi mwaka huu na miaka ijayo ujilete karibu,okay kama bado. Pia ibada zote – iwe ni ibada za maombi na maombezi usikose, ibada za sifa na kuabudu pia. Kwa kifupi uwe karibu na kanisa.
02.ujitenga na baadhi ya watu .
Kuna ufanikiwe ni lazima kuna aina fulani ya watu uwaache au ujitenge nao. Kwa maana si kila mtu atakusaidia katika safari yako ya mafanikio. Wapo ambao utakaowahitaji lakini wapo pia ambao hautawahitaji.
Hii ni kanuni muhimu sana ya kuzingatia kwa maana kama utajitajidi kwenda nao wote katika safari basi uwe na uhakika unaweza ukafika Kwa kuchelewa au usifike. Ebu jifunze kwa Paulo na Barnaba watu ambao walitengana. Lakini kutengana kwao ndio mafanikio kwa kila mmoja. ( Matendo 15:36-41)
Lakini pia jifunze kwa Ruthu mwanamke ambaye alimwachilia Orpa arejee nyumbani ili yeye asonge mbele. ( Ruthu 1:15). Labda kama wangelienda safari moja na Orpa wangekwazana njiani.
Hata kwako kuna watu ambao lazima uwaachilie waende njia zao,nawe usonge mbele. Shida kubwa iliyopo hivi Sasa,ni kwamba unataka uende na wote hao,umewashikilia wote ukidhani watakuwa msaada kwako.
Ukumbuke wengine si wema,na wengine watakukwamisha katika safari yako. Sina maana uwe peke Yako,bali nina maana ya kukubali kuwapoteza baadhi ya watu katika safari yako ili utimize ndoto yako katika mwaka huu na miaka mingine ijayo.
Hivyo vijana wengi ni watu wa makundi, lazima ukubali kujitenga na makundi kwa maana wewe sio wao,wapaswa kuangalia mambo ya kwako binafsi.
03. Komboa wakati.
Kila kitu kimefungamanishwa na muda. Suala la kutimiza ndoto yako linahusu muda. Hivyo,ukijua kutunza na kukomboa wakati, hakika utakuwa mahali salama zaidi kuelekea kutimiza ndoto yako. Kumbuka “muda haupotezwi bali unatunzwa” hivyo epuka kupoteza muda katika mambo yasiyo muhimu kwako. Mfano kutumia muda mrefu katika mitandao ya kijamii,ni kupoteza muda ( unless uwe na kitu muhimu), kutumia muda mrefu katika luninga/ Television -TV, n.k
Jamaa(Deo mnyamwezi) alikuwa mtu wa maskani sana. Mahali ambapo wanapoteza muda mwingi wa kukaa na kuanza kuota ndoto za kufika mamtoni/ulaya wakati hata passport tu hawana. Maskani imekula muda mwingi wa Deo,kiasi kwamba kufanikiwa kwake kunakuwa kigumu! Jifunze hapo,usije ukafanana na Deo Kwa kupoteza muda kukaa maskani na washkaji bila sababu yoyote.
Biblia inatupa mfano mzuri juu ya watu ambao walikuwa hodari,watu wenye akili za kujua nyakati,hawa walikuwa ni wana wa Isakari ( 1 Nyakati 12:32).Nawe lazima uzijue nyakati,ujue vizuri kutumia muda wako ipasavyo. Hapo ndipo utaona ukielekea kwenye kusudi lako.
04. Fanya kazi kwa bidii.
Moja ya Jambo muhimu litakalokusaidia ni kujituma katika kazi. Kila kazi upatayo,uifanye Kwa moyo na bidii kama Kwa Bwana ( Mhubiri 9:10). Tunaposema “ufanye kazi kama kwa Bwana ” Nina maana;Kila kazi upatayo kufanya uifanye kwa uaminifu mkubwa kana kwamba ni kazi ya kanisa. Na kuifanya kwa ufanisi.
Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900
Namba ya what’s app ni .+255 746 446 446
Mchungaji Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comments