top of page

MUNGU ATAKUOKOA.

Updated: Sep 5, 2022




“Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,Kwa kuwa amenijua Jina langu.” Zab.91:14

Neno “kukaza” lina maana ya kungangana katika kuendelea bila kuchoka au kukata tamaa. Hivyo ukikaza kumpenda Bwana unakuwa na hali ya kuendelea kujitoa kwake bila kukata tamaa wala kuangalia mambo mengine yote. Ni kweli kwamba,ukikaza kwa Bwana,Bwana atakuokoa. 


Mstari huu,umebeba uwajibikaji wako mbele za Mungu na kisha ndipo uokolewe. Kuokolewa kunakozungumzwa hapa ni zaidi ya maana ya kuokoka kwa kumpokea Yesu Kristo kwa maana kuokoka kwa kumpokea Yesu Kristo ni neema kwa njia ya imani, bali hapa haizungumziwi neema,bali jitihada na juhudi zako za kumpenda Mungu baada ya kupokea neema


. Ni lazima ujue kwamba hapo kuna aina fulani ya kanuni ya makubaliano baina ya pande mbili, kati yako na Mungu;kanuni hiyo inategemea na kiwango chako cha kumpenda Mungu. Hii ina maana kwamba kulikuwa hakuna nafasi ya kuokolewa au kuinuliwa,lakini kwa sababu umekazana kumpenda Mungu,basi kwa bidii yako Mungu amelazimika kukuokoa. 

Hivyo,katika andiko hilo,inaonesha wazi kwamba kile kilichomfanya Mungu kumuokoa mtu huyo ni “bidii yake isiyokoma kumpenda Mungu” na si kinginecho. Vivyo hivyo kwako,


inawezekana kabisa ukawa huna sifa za kuinuliwa au kuokolewa lakini kwa bidii ya kujidhabihu ndio itakuinua. Hivi umeshawahi kumuona mtu ambaye hana sifa za kupata jambo fulani,lakini kwa sababu ya kujitoa kwake bila kukata tamaa kunamfanya apewe jambo hilo. Ndivyo neno la leo linavyokutaka uendelee kukaza kumpenda Mungu ili uokolewe na kupandishwa. 


Kwa mujibu wa andiko hilo,tunajifunza kwamba Mungu anaangalia uwajibikaji wako wa “kumpenda Yeye” ndipo akuokoe kwa maana ya kuinuliwa.  Kukaza kwako kwa ajili ya Mungu,ujue Mungu atakuokoa. Kuna mambo mengi ambayo yamkini hukumuomba Mungu lakini unashangaa Mungu akikutendea kwa sababu wewe unampenda sana Yeye,Mungu anapoliona pendo lako kwake,basi Yeye atakutendea tu.


Kumpenda Mungu ni kulishika neno lake (kuliishi neno la Mungu)~ Yoh. 14:23.  Kuna gharama katika kulishika Neno la Mungu.


Ni wale tu waluokoka na kuyakataa matakwa yao ili mapenzi ya Mungu yafanyike kwao. Si neno dogo kuliishi neno bila kuwezesha na Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu,kamwe huwezi. Nimegundua kwamba kuna kazi ya ziada ili Bwana akuinue,….


Kwa mawasiliano pamoja na what’s app number +255 746 446 446


ITAENDELEA…

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page