MTU USIYEMJUA MWENYE KUTEMBEA NA WASAA WA HATMA YAKO – 03 (Tamati)
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 16, 2020
- 5 min read
Updated: Sep 29, 2022

Na Mwl.AndreaG.Muhozya.
…What am I saying? Nasema hivi. Mtu usiyemjua anapokuja maishani mwako BE CAREFUL. Hata kama amekukatisha usingizi mtamu au amekurushia likitambaa lenye majasho yake huku wewe ukiwa busy na kazi. Watu wengi wameyapenda maisha yao kuliko DESTINY zao na hivyo kupoteza kila kitu. Wanakufa moyoni wakiwa hawana amani yoyote. Be careful.
Hii ni sauti ya Mungu inakuja kwako kupitia maandishi haya. Kuwa makini usipishane na destiny yako. Elisha aliishi DESTINY yake kwa sababu alitambua majira ya kuijiliwa kwake. Na akadestroy PRESENT NA PAST ili ASIPOTEZE FUTURE.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Haya.
Twende mbele totoke enzi za Eliya.
Enter the MASTER.
Jesus of Nazareth.
Huyu sasa si mchezo. Funga kazi. Imagine one day yuko anapita zake akakuta mtu yuko “TRA” anafanya kazi zake. Then akamwambia tu: “NIFUATE” Mtu yule akaacha kila kitu na kumfuata.Unadhani ni rahisi?
Yaani umesoma umepata kazi TRA halafu anapita stranger tena anatembea kwa mguu hana hata ka-Vitz. Anakwambia neno moja tu: NIFUATE. Unaresign kazi siku hiyo hiyo kumfuata mtu usiyemjua ili uende naye USIKOKUJUA.Mathayo hakusikia neno FOLLOW ME. No. Alipomtazama Yesu as a stranger aliona destiny yake imetandikwa mbele yake.
How?
Instinct. Instinct inamwambia TRUST THIS MAN. Hapo akili haifanyi kazi. Kama hujafikia hatua ya instinct yako kuwa kali kuliko brain yako utamiss destiny yako. Utapishana na wakati wa kuijiliwa kwako kwa kuwa utamdefine STRANGER kwa BRAIN kwa kuwa huna instinct itakayokwambia TRUST THIS PERSON.
Petro, Yohana, Yakobo waliziacha NYAVU (BUSINESS ZAO) wakaanza kutembea kwa mguu na stranger. Walitambua kuwa kumbe muda wote waliokuwa baharini ilikuwa ni TRAINING TU. Kazi yao ilikuwa ndo inapaswa ianze. Wakaacha wakamfata Yesu. Kufanya kazi BOT au VODACOM au BBC au popote pale inaweza kuwa training tu Mungu alitaka upitie huko. Wewe umeigeuza kuwa ndo DESTINY yako!
Kumbuka kina Mathayo, Petro, Yakobo na Yohana na wengine wengi.
Kuna mtu ana mashaka leo na ukuu na kujulikana kwa Yakobo, Petro, Yohana, Mathayo?Yesu aliondoka. Wao wakabaki na kufanya makubwa. The stranget will leave. But your destiny will stay.Kuna watu wangapi walimwona Yesu kama stranger tu na si kama mtu aliyebeba DESTINY ZAO.
Wengi! Yesu aliwaambia watu wengi tu neno lile lile:”NIFUATE”
Wengine wakasema: “SAWA LAKINI UNAJUA NIMEFIWA SO NGOJA NIKAZIKE THEN NITAKUJA”.
Story zao zikapotelea hapo mpaka kesho. Greatness ambayo Yesu aliiona ndani yao ikafia hapo. Kumbuka your destiny is tied to someone who must guide you at least for a while.
Wengine walimjibu Yesu: NGOJA NIKAAGE…. NGOJA NIKAOE KWANZA…. NGOJA KIDOGO MKUU…. NGOJA NIKAJIPANGE SI UNAJUA SIWEZI KUKURUPUKA?….😆 NGOJA NIMALIZE SHULE SI UNAONA MI BADO MDOGO? Nk nk.Na mpaka leo majibu ni hayo hayo.
Yeremia aliwahi kusema hivyo pia.
“Mimi bado mdogo”.Mungu akamhurumia tu bure na kumjibu tu USISEME MIMI MDOGO. (Coz unanifanya mimi Mungu nionekane sijui nachokifanya hadi kukuita wewe.
I see something in you regardless of your age, or education or background. So usinifanye mimi sijui umri wako” So… Wake up people!
Usipishane na STRANGER WAKO ndugu. Utajilaumu and it will be too late. Elisha angeachana na Eliya tusingemjua. Be alert. Petro angemkimbia Yesu ingekula kwake siyo kwetu. Yesu angechagua mwingine tu. Una get?
Kuna watu walikuwa wanafunzi wa Yohana mbatizaji. Yesu akipokuja walimwacha Yohana wakamfuata Yesu. Walijua kwa Yohana ilikuwa trela. MOVIE ndo imeanza. But kuna watu wakabaki na Yohana mbatizaji hadi akakatwa kichwa wakabaki kwenye mataa. Tambua NYAKATI. Be alert when a stranger shows up.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Okay.. Enzi za Yesu nazo basi mbali. Tuje enzi za Karibuni zaidi. Marekani kuna vijana wasiojuana walikutana shuleni. Wakajenga urafiki. Wakasoma hadi ngazi ya chuo. Vyuo tofauti. Mkubwa akaacha chuo akaanza kufanyia kazi ndoto yake. Baadaye akamshauri mdogo aache chuo chake pia waanzishe kampuni. Mdogo akawaka moto ndani. INSTINCT. Akaacha chuo. Harvard. Unaachaje Harvard yani? We chizi?
No siyo chizi. Nimetambua wakati wa KUIJILIWA KWANGU.
So wakaachana na elimu ya juu. Wakaanzisha kampuni mwaka 1975. Mkubwa aliitwa Paul Allen. Mdogo ni Bill Gates. Microsoft ni jina alilotunga Paul Allen. Paul Allen aliondoka Microsoft mwaka 1982. Amefariki mwaka jana 2018. Lakini Bill Gates ndo anajulikana zaidi hadi leo na amefanikiwa zaidi. Listen. Narudia. The stranger will pass. But your destiny will remain.
Kama umeshapoteza stranger wako mkimbize aliko kama Elisha. Na uombe Mungu awe anakungoja kama Eliya alivyomngoja Eliya. Au kama kama kaka Aaron pale Mwanza station alivyozidi kunisemesha kwa upole vile vile licha ya kuona nimekereka.
Chase your stranger. Akipotea in your life utaishi empty life no matter magari mangapi utakuwa nayo.
Mfano mwingine. Unamjua mtoto yoyote mwenye miaka 11? Basi miaka mingi iliyopita kuna katoto kadogo huko Marekani kalipenda kusoma vitabu. Kakawa kanashinda maktaba kusoma. Kakapenda sana topic ya uwekezaji. By the time kana miaka 11 kalikuwa kameshasoma vitabu vingi juu ya uwekezaji kupitia maktaba huko Omaha jimbo la Nebraska. Nadhani utakubaliana na mimi kuwa vitabu vingi utakavyosoma maishani vimeandikwa na STRANGERS na siyo shangazi zako au baba mkubwa. Strangers.
Akiwa na miaka 19 huyu dogo akakutana na kitabu kwa BAHATI TU. Kitabu cha stranger mwingine anaitwa Benjamin Graham kitabu kinaitwa THE INTELLIGENT INVESTOR. Kuna kitu ndani ya huyu dogo kikasema hii ndo lulu ambayo itakubadilisha. LISTEN TO THIS MAN. Dogo akasoma hicho kitabu takribani mara sita.. Na akaanza kufanyia kazi yaliyomo humo. Huyo “dogo” ndiye Warren Buffet. Tajiri namba 3 duniani ambaye amefanikiwa mno kupitia uwekezaji na anasema siri yake ni hicho kitabu.
You get it?
Mifano ni mingi. Muda hauruhusu. Duniani kote greatness ina mchango mkubwa kutoka kwa STRANGERS. Chunguza utaona. Na utashangaa. Awe Gandhi, awe Nyerere awe Mandela awe Christopher Columbus, awe JPM awe Ronaldo au Messi awe Michael Jordan au Oprah. Kuna encounter na stranger iliyobadili maisha yao.
Robert Kiyosaki alipata hiyo encounter kwa baba wa rafiki yake. Hivyo siyo ndugu wa kuzaliwa. Ni mtu baki tu. Anaitwa mzee Richard Wassman Kimi ambaye actually ndiye RICH DAD wa vitabu vya Kiyosaki. Alikuja maishani mwake na kupita but leo hii Robert Kiyosaki yupo na anamiliki Real Estate properties zaidi ya 5000 duniani hoteli 3 kubwa na golf courses za maana 5 (si unajua wanaocheza golf ni kina nani). Ushauri wa baba wa rafiki yake ulimchoma moyoni kuliko ushauri wa babake mzazi. Kuna kitu kilimwambia Kiyosaki
TRUST THIS MAN. LISTEN TO THIS MAN.
My friend hicho kitu kikikosekana utaamini umbea wa Instagram na kupoteza muda ukifatilia maisha ya Wema Sepetu mpaka siku unakufa.Nimewaka moyoni mwangu kukupa ujumbe huu nikaona nikufikishie nisije kudaiwa.
Usipishane na stranger wako kwa kujaribu kutumia akili mahali ambapo kuna kitu moyoni mwako kinakwambia ACHA KILA KITU MSIKILIZE HUYU. Laiti ungejua njia za Mungu za kukukutanisha na wakati wa kuijiliwa kwako usingethubutu kuwachukulia watu poa. Mungu anapomleta huyo SPECIAL stranger in your life utaona tu anaongea na wewe TOFAUTI na ulivyozoea kusemeshwa. In a way ambayo utaona tu kuna utofauti mkubwa. Mungu yuko interested na wewe zaidi ya huyo stranger. Stranger ni mtumishi tu.
Messenger.
Narudia THE STRANGER WILL PASS BUT YOUR DESTINY WILL STAY
Don not miss your kaka Aaron kwa kupenda usingizi Do not miss your Elijah kwa kukereka kirahisiDo not miss your Jesus kwa kumwona hana hata Vitz. (“Motivational Speakers” wanaoanza hukutana sana na hili.
“Unatwambia nini wewe huna hata Vitz”. Stay focused son. Yesu alikuwa kwa mguu muda wote hana hata pa kuishi)
Again… Do not miss your Paul Allen kwa kumwona ana haraka ya maisha Do not miss your Benjamin Graham kwa kusema hawa waandishi wanaongea tu.
Rafiki. Don’t miss that book kwa uvivu tu wa kusoma. Kuna kitabu ulinunua miaka mitano sasa unacho tu. Hujui huyo stranger kwenye shelf huenda ndiye Benjamin Graham wako. Utainyima dunia mambo makubwa mno usipofanikiwa. Na utadaiwa I promise you.
Kumbuka hilo unapoianza 2020.
Do not miss your destiny kama walioenda kuzika au kuoa au kuaga wazazi nk wakamaliza hayo na kukuta Yesu keshafunga chapter ya kufanya nao kazi. They missed an opportunity of their life. That’s the biggest loss of life. To miss your destiny moment. So rafiki….
Who is your Aaron? Who is your Elijah? Who is your Jesus? Who is your Paul Allen? Who is your Benjamin Graham?
Stay alert. Stay awake.
Nakupenda. Nakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2020 nakuombea usikose destiny yako. Usipishane na kusudi la kuja kwako duniani. Usimpotezee Eliya wako hata kama amekudistract na kakukera kwa kukurushia likitambaa ukiwa busy na kazi zako. Ona zaidi ya hilo likitambaa lenye majasho. See beyond the “distraction”.
See beyond that stranger.
TAMATI !
Ikiwa umebarikiwa,tufahamishe tumtukuze Mungu pamoja,kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa;
Semper Fidelis,
Andrea G. Muhozya Entrepreneur & Business Trainer Dar es Salaam, Tanzania East Africa +255 788 366 511. Na + 255 683 877 900 :::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Comments