top of page

LANGO LA NDOTO – 1

Updated: Aug 26, 2022

Tafsiri ya neno “ndoto” kibiblia ni mlango wa mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu katika ulimwengu wa roho wakati mwanadamu alalapo. Ndoto ni moja ya njia ya mawasiliano ya kiroho ya karibu na haraka ambayo Mungu anayoyatumia kufikisha ujumbe wake kwa mhusika. Hivyo ndoto ni kama madhabahu anayoitumia Mungu kusemea kwa watu wake kwa haraka.


Angalia mfano pale Mungu alipotaka kusema na Yusufu kwa haraka juu ya hatari iliyokusudiwa na Herode juu ya mtoto Yesu,Mungu alitumia lango la ndoto na kumfunulia Yusufu kuhusu mabaya yote yaliyopangwa naye Yusufu alipoamka usiku huo huo akafanya haraka kukimbia mji na mtoto Yesu pamoja na Mariamu ( Mathayo 2:13)


Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.” Hesabu 12:6


Angalia hilo neno “..nitasema naye katika ndoto…” Huyo ni Bwana Mungu anayethibitisha kwamba Yeye husema na mtu amtakaye katika ndoto tena bila mipaka. Hivi unajua Mungu hana mipaka ya kusema nasi katika ndoto,Bali sisi ndio tunajiwekea mipaka hata inafika wakati tunasema “ukiwa haujaokoka au ukiwa mwovu Mungu hawezi usema nawe,” lakini huo ni mtazamo wa kitoto,kwa maana ukifahamu kwamba Mungu hana mipaka basi huwezi kuwa na mtazamo huo au kusema hivyo.


Kwa sababu biblia inatuambia Mungu alisema na Farao ambaye alikuwa mungu mtu/mtu mwovu kupitia lango la ndoto ( Mwanzo 41:32)na ndio Mungu huyo huyo anayesema na wateule wake hata sasa. Hilo ni jambo muhimu la kuelewa kwamba Mungu husema bila mipaka katika ndoto.


“Ndoto” ni jambo la ajabu na la kushangaza sana ambalo hakuna mwanadamu mwenye kujua hasa nini kinachoendelea kwenye ufahamu wa mtu aliyelala hata akaota,ajuae ni Mungu tu. Hata kitendo cha kulala tu,ni muujiza tosha kwa maana alalaye hajui kwanza muda kamili kwamba kalala saa ngapi? yupo wapi ? maana ni kama vile mekufa ! Nini kitamfanya arejee tena katika hali yake ya kwanza / kuamka!!!


Vivyo hivyo “ndoto” ni kitu cha kipekee maana wakati mtu amekuwa kama kafa tena akili zake hazina akili tena / hazina matunda hapo ndipo anapata picha zinazotembea kama movie hivi,naye aweza akajiona katika movie hiyo ama kuona mambo mengine mengi.

Ukijiuliza imerekodiwa saa ngapi ,au wapi,? Hakuna majibu !!! Inakuawaje kuwaje hata ukaweza kuona picha katika ufahamu ikiwa mtu kalala bila kujijua.


Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;” Ayubu 33:14-15.


Kwa mujibu wa andiko hilo la Ayubu tunaweza kujifunza mambo machache katika lango la ndoto kama ifuatavyo;


  1. Mungu hunena mara nyingi zaidi katika ndoto.


Ni kawaida ya Mungu kunena nasi mara nyingi zaidi katika hali ambayo tutaelewa kwa wepesi. Hufanya hivyo pia katika ndoto na ndio maana hunena zaidi ya mara moja, neno linasema“Mungu hunena mara moja,Naam hata mara ya pili..” Neno “hata mara ya pili” ni kuonesha upendo wake kwetu. Ili kusudi kama hatujasikia mara ya kwanza basi mara ya pili tuweze kusikia.


  1. Hali ya kutokujali ya mwanadamu.


“…ajapokuwa mtu hajali.” Ni tabia ya wengi kutokujali neno la Bwana. Hali ya kutokujali ni kitendo cha kupuuzia au kutokufuatilia. Ebu jiulize wewe mwenyewe tu,ni mara ngapi Bwana amekuwa akikusemesha katika lango la ndoto lakini wala hujali? Tena wala hushtuki!!! Jiulize tu,ni mara ngapi Bwana amekuwa akikuonesha mambo makubwa ndotoni lakini hukuchukua hatua yoyote ?


Kuna watu ambao Bwana amekuwa akitumia lango la ndoto kuwataarifu mambo mengi mengine ni mambo ya kutisha lakini kwa sababu ya kutokujali,basi watu hao hata hawaangaiki na chochote yaani hata kutafuta maana tu ya ndoto hizo hawafanyi,hawajali.!!!


ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja,na kwa msaada zaidi piga +255 683 877 900.


What’s app +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Recent Posts

See All

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page