top of page

FAHAMU MIUJIZA YA YESU.

Na Mch Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Hakuna aliyetenda miujiza mingi na ya kushangaza kama miujiza aliyotenda Yesu. Alitenda,ametenda na anaendelea kutenda kila siku na ataendelea kutenda na kutenda. Bwana amenitendea mimi mambo makuu ya ajabu na ndio maana nami nataka nikujuze maajabu haya. Kama ametenda kwangu,atatenda na kwako pia ni kuendelea kuweka imani yako kwake Yesu. Ni kweli umekuwa ukingoja Bwana akuinue lakini nataka nikuambie tu,Mungu yupo na atakutendea.Leo,ebu nikufundishe miujiza ya Yesu michache kati ya mingi. Kwa mujibu wa biblia tunaweza tukaigawa kwenye makundi makubwa matatu kama ifuatavyo;

  1. Miujiza ya uponyaji.

  2. Miujiza ya kudhihirisha nguvu ya Mungu dhidi ya vitu / mambo ya asili

  3. Miujiza ya kufufua.

Ifahamike kwamba “miujiza” ni moja ya karama katika zile karama tisa ( 1 Wakorintho 12:8-10). Ingawa miujiza ni karama ya Roho mtakatifu lakini Yesu alitaka watu waweze kuketi katika neno na wasimtafute kwa sababu ya miujiza bali neno ( Yoh 6:26). Hii ina maana kwamba,miujiza inapaswa itokane na neno halisi ( Marko 16:20). Kwa sababu miujiza haituingizi mbinguni isipokuwa neno lake Bwana hutukuza hata kuwa na mahusiano mema na Mungu wetu na hapo ndipo kwenye kuiona mbingu. Miujiza ni lazima iwepo siku zote panapokuwa na neno halisi la Bwana,kamwe haiwezi ikafichika wala hutaitaji kutumia nguvu zako bali Bwana atatenda maana kuna neno lake,Yeye huliangalia neno lake.

Katika miujiza ya Yesu,ni “miujiza ya uponyaji ” ndio ilikuwa mingi ukilinganisha na miujiza mingine. Huyu hakuwa mwanadamu tu bali Mungu maana matendo yake yashangaza. Hata sasa Yesu anaponya kwa sababu yu hai. Wewe ni shahidi mkubwa wa mambo haya ninayokuandikia,ni mara ngapi unashuhudia uponyaji unaendelea kufanyika katika Jina la Yesu? Ni mara nyingi sana maana hata leo amekusudia kukuponya wewe na mwingine na mwingine. Hivyo ebu sasa nikupitishe kwenye makundi haya ya miujiza ya Bwana;

01.Miujiza ya uponyaji.

  1. Uponyaji kwa mama mkwe wa Petro ( Mathayo 8:14-15,Marko 1:30-31,Luka 4:38-39)

  2. Mwenye ukoma (Mathayo 8:2-4,Marko 1:40-42,Luka 5:12-13)

  3. Mtu aliyepooza ( Mathayo 9:2-7,Marko 2:3-12,Luka 5:18-25)

  4. Mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu miaka kumi na miwili ( Mathayo 9:20-22,Marko 5:25-29,Luka 8:43-48)

  5. Watu wa wiwili kutoka katika nchi ya Wagerasi ( Mathayo 8:28-34,Marko 5:1-15,Luka8:27-35)

  6. Mtumishi wa akida wa kirumi (Mathayo 8:5-13,Luka 7:1-10) -Muujiza huu ulikuwa ni wa ajabu,maana hajatokea katika Israeli imani kubwa namna hii.

  7. Mtu bubu mwenye pepo ( Mathayo 9:32-33)

  8. Kiziwi na bubu  ( Marko 7:31-37)

  9. Kijana mwenye pepo (Mathayo 17:14-18,Marko 9:17-29,Luka 9:38-43)

  10. Vipofu wawili pamoja na Bartimayo mwana Timayo (Mathayo 20:29,Marko 10:46-52,Luka 18:35-43)

  11. Vipofu wawili ( Mathayo 9:27-31)

  12. Mtu mwenye pepo ndani ya Sinagogi ( Marko 1:23-26,Luka 4:33-35)

  13. Yule kipofu kule Bethsaida ( Marko 8:22-26)

  14. Binti (aliyepagawa na pepo siku nyingi) wa mwanamke Mkananayo ( Mathayo 15:21-28,Marko 7:24-30)

  15. Kipofu na aliyekuwa bubu mwenye pepo ( Mathayo 12:22,Luka 11:14)

  16.  Mtu mwenye mkono uliopooza ( Mathayo 12:10-13,Marko 3:1-5,Luka 6:6-10)

  17. Mwanamke aliyekuwa na pepo la udhaifu,pepo alimpinda ( Luka 13:11-13)

  18. Mtu mwenye ugonjwa wa safura ( Luka 14:1-4)

  19. Wakoma kumi (Luka 17:11-19)

  20. Mtumishi wa kuhani mkuu (Luka 22:50-51)

  21. Mtoto wa diwani aliyekuwa mahututi kufa (Yohana 4:46-54)

  22. Mgonjwa wa miaka 38 huko kwenye kisima Bethsaida  ( Yohana 5:1-9)

  23. Kipofu wa kuzaliwa ( Yohana 9:1-7)

02.Miujiza ya kudhihirisha nguvu dhidi ya mambo yanayotuzunguka ( mambo ya asili)

  1. Kutembea juu ya maji ( Mathayo 14:25,Marko 6:48-51,Yohana 6:19-21)

  2. Kutuliza gharika ( storm) ( Mathayo 8:23-27,Marko 4:37-41,Luka 8:22-25)

  3. Kuwalisha watu 5,000 ( Mathayo 14:15-21,Marko 6:35-44,Luka 9:12-17,Yohana 6:6-13)

  4. Kuwalisha watu 4,000 (Mathayo 15:32-38,Marko 8:1-9,)

  5. Shekeli kwenye mdomo wa samaki ( Mathayo 17:24-27)

  6. Mtini aliyeulaani ( Mathayo 21:18-22,Marko 11:12-14,20-25)

  7. Uvuvi wa samaki wengi ( Luka 5:4-11)

  8. Maji kuwa divai ( Yohana 2:1-11)

  9. Uvuvi mkubwa tena,samaki wengi baada ya kufufuka kwake Yesu ( Yohana 21:1-11)

03. Miujiza ya kufufua wafu.

  1. Binti wa jumbe kufufuliwa ( Mathayo 9:18-19,23-25,Marko 5:22-24,Luka 8:41-42,49-56)

  2. Maiti kwenye mji wa Naini ( Luka 7:11-15)

  3. Lazaro (Yohana 11:1-44)

Katika miujiza hiyo,ni michache maana hata biblia haikuandika mambo yote aliyoyafanya Bwana,sababu kama yangeliandikwa yote biblia isingelitosha ( Yohana 21:25). Hivyo katika miujiza hiyo iliyopata kuandikwa,mambo yafuatayo unaweza kugundua;

  1. Muujiza wa kuwalisha watu watu 5,000 wanaume bila wanawake na watoto ndio muujiza pekee ulioandikwa na wainjili wote wanne ( Wainjili hao ni Mathayo,Marko,Luka na Yohana) angalia hapo juu kwenye kundi la pili la miujiza.

  2. Luka ameandika miujiza mingi ya uponyaji kuliko wote.

  3. Miujiza ya uponyaji iliyoandikwa na Yohana,ni yakipekee ambayo haijawahi kuandikwa na wengine.

Kumbuka;

Yesu yu hai hata leo na anatenda kazi hata sasa,ukimuamini Yeye hakuna kinachoshindikana kwake ( Marko 9:23). Natamani tuombe pamoja leo katika maeneo unayopitia sasa ili Mungu atende leo kwako kama ilivyoandikwa. Ukiamini inawezekana. Na ikiwa kama umejifunza kitu basi usiache kunipigia simu leo nipate kujua.nipigie sasa kwa namba hizi;+255 683 877 900.

Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446

Mch. Gasper Madumla.

S.l.P 55051 DSM,TZ.

Beroya bible fellowship church( Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page